Taasisi
binafsi ya KWA PAMOJA TUNAWEZA yajiandaa kuanzisha shindano litakalokuwa na
kauli mbiu MAMA AFRIKA litakalokuwa na kauli mbiu “Mwanamke hasifiwi sura
anasifiwa Maendeleo” linalolenga kumuibua mama atakayekuwa mfano wa kuigwa kwa
wanawake wengine (kioo cha jamii) tunapoelekea mwaka 2030 ambapo sifa zifuatazo
zitazingatiwa.
Mwadilifu.
Mwajibikaji.
Mwenye
huruma na Upendo.
Mwenye
ubunifu.
Mwenye
maono.
Mwenye
hofu ya Mungu.
Mwenye
ujasiri wa kuthubutu.
Mwenye
kujali Jamii na Kutunza Mazingira.
Kiongozi wa Twaweza Bi. Sadah Akiongea mapema leo.
Kutokana
na sifa hizo shindano hilo litaanza kwa mkoa wa Dar Es Salaam wilaya ya
Kigamboni na kuendelea wilaya nyingine Ilala, Temeke, Ubungo na Kinondoni kisha
watashindanishwa na baadaye kumpata “MAMA AFRIKA 2030”.
Katika
majukumu hayo yatahakikisha anafanya na kubuni njia mbalimbali kwa kushirikiana
na wadau wengine njia za kuwainua kifikra na kiuchumi kwa wanawake wa eneo
husika.
Shindano
hilo litaendeshwa kwa mara ya kwanza kuanzia wilaya ya kigamboni tarehe
03/09/2016, huku baadhi ya makundi katika jamii yakionekana siyo sehemu ya
jamii, mfano ni pamoja na wale wanaoitwa “DADA POA” hivyo dada hawa wanatakiwa
kuwezeshwa kifikra na kiuchumi, si kwa kutumia nguvu ila kwa sababu kufanya
hivyo ni kudhalilishwa utu wa mwanamke hususani wa kitanzania.
Vilevile
kundi lingine ambalo limelengwa katika shindano hilo ni “MAMA WA NYUMBANI”
ambao hutebemea kuwezeshwa kwa kila kitu na endapo mume akiumwa au kufariki
wanapata matatizo makubwa kwa kuwa walishazoea maisha tegemezi.
Post a Comment