0


Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifungia gazeti la mseto, ikiwa ni hatua inayotokana na uandishi usiofuata taaluma ya uandishi.

Amri ya kulifungia gazeti hilo imetolewa kwa tangazo la serikali No.242 lililotolewa tarehe 10.August 2016, ambapo uamuzi umetolewa kwa kujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 sura ya 226 kifungu cha 25 (1), hivyo kutokana na amri hiyo gazeti hilo litakoma kutolewa tangu siku/tarehe ya kuanza kutumika na itakayotajwa katika amri hiyo.

Uamuzi huo unazuia gazeti la mseto kuchapishwa katika njia yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (online publication) kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya kieletroniki na posta sura 306.

Aitha, hatua hiyo ya kulifungia gazeti hilo imechukuliwa baada ya msajili wa magazeti kufanya juhudi za muda mrefu toka September 2012 – August 2016 kumtaka mhariri wa gazeti hilo kuacha kuandika habari za upotoshaji, uchochezi na za uongo, zisizo zingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Kutokana na hali hiyo, serikali kwa masikitiko makubwa, imelazimika kuchukuan uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo wa kuandika na kuchapisha habari ya uongo na kughushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za serikali kwa nia ya kumchafua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dtr John Pombe Magufuri na Viongozi wa serikali, kwa lengo la kutaka kumchonganisha na wananchi ambao wamekuwa na matarajio makubwa kwa uongozi wa awamu ya tano.

Pamoja na serikali kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayoainisha uhuru na mipaka ya habari, kama vile tamko la kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948, mikataba na matamko hayo kwa pamoja licha ya kuainisha uhuru wa habari ambao Tanzania imeruhusu kwa kiwango kikubwa, pia imeweka ukomo wa uhuru kwa kukataza habari za uongo, uzushi na uchochezi.
Serikali itaendelea kujenga uhusiano mzuri na wa kirafiki kati yake na wadau wa sekta ya habari. Hata hivyo mh. Waziri anasisitiza wadau wa sekta ya habari kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya taaluma ya uhandishi wa habari ili kujenga heshima ya tasnia ya uandishi wa habari na kulinda Amani ya nchi yetu.

Post a Comment

 
Top