0




Kufuatia kauli zinazosemekana za kichochezi zilizochapishwa na gazeti la Mwanahalisi la wiki tatu zilizopita kutoka tarehe 25 mpaka 31 July 2016 ambapo mwandishi wa nakala hiyo Mbunge wa Ubungo kupitia Chadema Said Kubenea aliyoiandika juu ya hali ya kukiukwa haki za kibinadamu Zanzibar, pamoja na kuwepo kwa shauli linalotokana na gazeti lililofungiwa la Mseto shauli hilo limewekwa kando, ikiwa na maana kesi yake ipo mahakamani.

Mbunge huyo alifika kituo kikuu cha polisi maeneo ya Stesheni majira ya saa 07:14 mchana ambapo alikaa kwa mahojiano mpaka 09:15 akiwa kaongozana na magari mawili ambapo gari aina V8 iliyokuwa imembeba yeye pamoja Mbunge wa singida mashariki Tundu Lisu iliruhusiwa kuingia ndipo walielekea moja kwa moja kwenye mahojiano.

Vilevile kufuatia jeshi la polisi kutaka kumuhoji mh kubenea juu ya gazeti hilo; mwanasheria aliyeongozana na Mh Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Chadema Mh. Lisu alisema “kutokana na sheria za magazeti kupinga mmiliki wa chombo hicho cha habari kuzungumzia anayepaswa kuzungumza au kuojiwa ni mhariri, mwandishi na mtoa habari”.

Hata hivyo mh. Kubenea yupo nje kwa dhamana ya Jeshi la polisi na anatakiwa kuripoti kituoni hapo alhamisi ya wiki ijayo kwa ajili maelekezo mengine ili kuamua kama mashitaka juu suala hilo yapelekwe mahakamani au hatua nyingine zaidi zichukuliwe.

Kufuatia hali hiyo naibu kamishna wa polisi kanda maalum Ezron Gyimbi amesema; wamemuhoji Kubenea juu ya maneno yake ya kichochezi na kutakiwa kufika, kulipoti kituoni hapo kwa hatua zaidi zitakazochukuliwa.



Post a Comment

 
Top