Wakati serikali ikiendelea kutoa rai kwa watumiaji wa barabara nchini, bado hali ya usalama kwa watumiaji hao inaonekana kutokuingia akilini huku baadhi ya madereva wakisababisha ajali hata maeneo ambayo ni nadra kiasi kuwepo kwa matukio hayo.
Majira ya 16:20 alasiri eneo la lugalo karibu na hospitali ya jeshi la wananchi Tanzania gari lenye namba T 765 APE lililokuwa likitokea maeneo ya mwenge na likiendeshwa na Kopro Charles Castory, lilipata ajali mara baada ya kuruka tuta lilipo barabarani hapo na kwenda kutumbukia kwenye mtaro, huku likimsababishia maumivu na majeraha afande huyo'
Kopro Charles ambaye ni mkazi wa Makongo juu, alikimbizwa kwenye hospital ya jeshi kwa kupewa huduma za dharula huku ikionekana akiwa na jeraha kichwani na sehemu ya kwenye paja la mguu wa kushoto likiwa na maumivu makali.
Chanzo cha ajali hiyo kilionekana ni mwendo kasi mkali ulisababisha kushindwa kupunguza mwendo katika eneo lenye matuta barabarani hapo
Chanzo cha ajali hiyo kilionekana ni mwendo kasi mkali ulisababisha kushindwa kupunguza mwendo katika eneo lenye matuta barabarani hapo
Mpaka mwandishi wa todayspro.blogspot anaondoka hospitalini hapo madaktari walikuwa wakimpatia huduma stahiki.
Post a Comment