ARUSHA.
Na. Leonard Mutani -Arusha.
Mamlaka ya Mapato nchini TRA imewataka wafanyabiashara wa sekta ya
utalii nchini kuendelea kuiamini serikali katika mfumo wa kodi uliopo sasa
pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali ambazo wafanyabiashara hao
wanakumbana nazo wakati wa ulipaji kodi.
PHOTO:
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere,
Akiongea wakati wa kufungua semina ya siku tatu kati ya TRA na waadau wa sekta
ua utalii mkoani Arusha mapema leo.
|
PHOTO: Wadau wa Sekta ya Utalii wakisikiliza
kwa makini hotuba ya kamishina mkuu wa mamlako ya mapato nchini (hayupo pichani)
ali[pokuwa akizungumza nao wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
|
PHOTO: Wadau wa Sekta ya Utalii wakisikiliza
kwa makini hotuba ya kamishina mkuu wa mamlako ya mapato nchini (hayupo pichani)
ali[pokuwa akizungumza nao wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
|
HABARI KWA UNDANI:
Akizungumza
kwenye semina ya pamoja iliyohusisha mamlaka ya mapato Tanzania na wadau wa
sekta ya utalii jijini Arusha, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Bw. Charles Kichere amewataka wadau hao kuelewa kuwa utalii ni sekta
muhimu sana, kwa hiyo kuwepo kwa sheria za kodi, taratibu na taratibu za kodi
ni muhimu sana katika kukua kwa maendeleo ya sekta hiyo.
Ameongeza kwa kusema “mwaka hadi
mwaka sekta ya utalii imekuwa ikihusika katika vipengere kadhaaa vya kukua kwa uchumi
wa nchi unakuwa kwa kasi, lakini pia serikali imeliona ombi la wafanyabiashara
la kutaka kulipa kodi kwa kutumia dirisha moja na mahala pamoja ili kuondoa
usumbufu wakati wa ulipaji wa kodi”
Vile vile kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maliasili na Utalii Deogratius Mdamu amesema kuwa kwa
pamoja idara ya utalii nchini ipo bega kwa began a mamalka ya mapato nchini ili
sekta ya utalii iweze kuchangia uchumi wa taifa.
"Tupo hapa kwa niaba ya serikali ili kuwasimamia wafanyabiashara
wa sekta ya Utalii kuwaelekeza ili waweze kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi hii” amesema Bwn. Mdamu
Kwa upande mwingine
akijibu swali kuhusu sekta ya Utalii nchini inachangia kiasi kidogo cha kodi Naibu kamishina wa oparesheni kodi za ndani Abdul
Bakari Zuberi amesema kuwa sekta hii ni ya tatu kati ya sekta tatu kubwa
zinazolipa kodi nchi pamoja na kwamba sekta ya utalii imekuwa ikikumbwa na
tatizo la uandikishwaji.
“bado kuna players wengi sana ambao wanashiriki kwenye sekta hii
ya utalii hawajaingia kwenye wigo wa kodi na ndiyo maana tumekuwa tukipiga
kelele sana ili watu waandikishwe, pamoja na kwamba hivi sasa tumeanzishwa
utaratibu wa kuwaendea watu kule walipo ili kuwaingiza kwenye mfumo”. Amesema Abdul.
Pamoja na hilo Mamlaka
hiyo inawatumia viongozi wa Serikali ikianzia na seikali za mitaa ili kujua
wale wote waanaofanya biashara pasi kujiandikisha ili wote waweze kuingizwa
katika mfumo wa ulipaji wa kodi.
Semina hiyo
inayofanyika jijini Arusha kwa siku tatu inategemewa kuwapa nafasi
wafanayabiashara hao wa sekta ya utalii kujadili na kutoa muelekeo wa kitaifa
katika ulipaji wa kodi ikiwa ni pamoja na kukumbushwa wajibu wa kulipa kodi husika kwa muda ulioamliwa na kuzingatia
matumizi sahihi ya mashine za EFD kwa ajili ya ushirikiano wa walipa kodi,
serikali na jamii kwa ujumla.
(Picha zote na Leonard Mutani) |
UPDATES:
Mamalaka ya mapato Tanzania (TRA) imezindua utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta ndogo isiyo rasmi (Machinga) mkoani Arusha.
Zoezi la utoaji vitambulisho hivyo linaongozwa na mkuu wa wikaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqaro akiwepo Mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro, mkurugenzi wa jiji la Arusha,. Loading....
Post a Comment