WACHAMBUZI, Watumishi wa umma na Wafanya biashara wakubwa nchini Kenya wanatathimini kwa ujumla matokeo ya hoja ya Rais Uhuru Kenyatta kufungua mipaka kwa Wananchi kutoka nchi nyingine za Afrika kuingia nchini Kenya bila passporti.
PHOTO: Rais wa Kenya Uhuru Jomo Kenyatta. |
Katika hotuba yake baada ya kuapishwa siku ya Jumanne, Rais Kenyatta alitangaza kufungua mipaka kwa wananchi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutafuta kazi, ardhi na makazi nchini Kenya.
Ikiwa hoja hiyo itatekelezwa, maelekezoyake yanamaanisha kwamba Waafrika wanaotaka kutembelea Kenya watastahili kupata visa kwenye bandari ya kuingilia, tofauti na siku za nyuma wakati wengi walipaswa kupitia mchakato mkali, mara nyingi wa gharama kubwa ili kupata visa katika mabalozi ya Kenya nje ya nchi.
Hata hivyo, hoja hii imeleta wasiwasi wa usalama huku mtaalamu mmoja akionya hatua hiyo ita leta sintofahamu kwa sababu mashirika ya usalama yatahitajika kufanya ufuatiliaji mkubwa zaidi kwenye maeneo yote ya mpaka.
Pia itamaanisha kwamba nchi hiyo itakabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya Waafrika wanaotaka kuingia, na hii itazipa changamoto kubwa huduma za uhamiaji.
Wakati nchi nyingine kama vile Rwanda zikiwa tayari zimefanya hivyo na hivyo kufanya uamuzi wa Kenya kuwa sio wa kwanza kabisa, tamko la Rais Kenyatta kuwa Wa afrika Mashariki watatendewa kama Wakenya bado linaelekea kuzungumzwa kote kwenye ukanda.
Wachambuzi wanakubaliana kuwa hoja hiyo itakuwa na athari kubwa katika nyanja za kijamii na kiuchumi, hasa, usalama, elimu, afya, kazi na ushirikiano.
Source: RFI
Post a Comment