ARUSHA.
Kongamano la siku mbili la wadau wa ununuzi na ugavi limemalizika na kufungwa rasmi na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, ambapo washiriki 583 kutoka mikoa mbalimbali nchini na baadhi kutoka nchi ya jirani ya Kenya walihidhulia.
PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwasili kufunga kongamano la wadau wa ununuzi na ugazi . |
PHOTO: Mwenyekiti wa Bodi ya ununuzi na Ugavi Dada Hellen Bandiho akiwatoa hotuba ya kufunga kabla ya kumkaribisha RC Gambo kufunga kongamano. |
PHOTO: Sehemu ya wadau na wanataaluma kutoka sehemu mbalimbali wakisikiliza hotuba ya kufunga. |
PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa hotuba ya kufunga kongamano |
PHOTO: Picha ya pamoja ya wataalam wa PSPTB wakiwa na RC Gambo. |
Katika hotuba yake amewataka wataalam hao kutumia weledi na uhaminifu ili kufikia malengo kwa taifa, kutokana na sekta hiyo ya ununuzi na ugavi kuwa kichocheo katika msingi wa uchumi wa taifa linalokua.
“zaidi ya asilimia 70 ya mambo yanayofanyika yanakwenda kwende ununuzi na ugavi, shughuli nyingi katika maofisi zinahusisha manunuzi na mambo mengine.” alisema Mrisho Gambo.
Aliongeza kuwa ikiwa wataalam wakizingatiwa na kupewa nafasi kufikiri na kwa kutumia weledi walionao, mabadiriko katika manunuzi yatakuwa makubwa zaidi.
Vile vile alisema mafanikio yoyote yatakayopatikana kutoka na wataalamu hao kutumia weledi na uaminifu wao wataifanya serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuri yenye kauli mbiu ya viwanda kufikia malengo na kuaminiwa kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya PSPTB Dada Hellen Bandiho amesema dhima kuu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu ni mchango wa wataala wa ununuzi na ugavi kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini.
Katika kongamano hilo mada mbalimbali kama; Mikakakti ya ukuzaji wa viwanda katika uchumi unaokuwa, Maendeleo ya viwanda Tanzania, Jukumu la wanunuzi wa wagavi na nyinginezo.
Pamoja na mikakati hiyo ambayo maazimio yake na taarifa yake yatawasilishwa katika mkutano wa tisa kwa mwaka unaokuja wa 2018, Alisema “tumechukua maoni ya wadau wote kwa lengo la kuboresha taaluma na kazi za bodi”
Aliongeza kuwa “tunawaomba wale wote waliopewa madodoso wajaze maomi yao ili kuboresha kazi za bodi kwa maendeleo yetu”
Dhamira ya Rais John Magufuri ni kuhakikisha nchi inakuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda, hivyo Dada Hellen amewataka wadau wote kufanya kazi kwa bidi ili kuweza kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda na kuleta maendeleo ya wananchinwa Tanzania.
Post a Comment