0
NAIROBI.
Mwanasheria Mkuu nchini Kenya Githu Muigai ameonya hatua ya kumuapisha Raila Odinga kama rais kuwa ni ya uhaini.
Akizungumza katika akiwa kwenye ofisi za Sheria Bw. Muigai alisema iwapo NASA itaendelea na mipango hiyo itakua inakiuka katiba na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya viongozi wa muungano huo wa upinzani.

Mwanasheria huyo Mkuu wa serikali ya Kenya Githu Muigai ameonya kuwa iwapo kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga ataapishwa wiki inayoanza kesho, atafunguliwa mashtaka ya uhaini.
"Aidha wanaoendesha shughuli za uundwaji wa mabunge ya wananchi pia wanakiuka Katiba na vilevile watachukuliwa hatua kali," amesema Githu Muigai.
Mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai, alisema kwamba ni uhaini wa hali ya juu kwa mtu yeyote kuapishwa kama rais wa nchi hiyo iwapo tayari kuna rais ambaye ameapishwa kwa mujibu wa katiba.
PHOTO: Mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai.

Muigai alikuwa akijibu tetesi zilizoshika kasi kwamba kiongozi wa muungano wa upinzani wa Kenya, Raila Odinga, ataapishwa kama "
rais wa wananchi' mnamo tarehe 12 Disemba.
Mwanasheria huyo aliwaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kwamba sheria za uhalifu nchini Kenya ziko bayana kuhusu hatua zinzofaa kuchukuliwa kwa mtu yeyote atakaye vunja sheria hiyo
Kauli ya Muigai imekosolewa na Mwanasheria Mkuu wa muungano wa upinzani NASA, Seneta James Orengo ambaye amepuuzilia mbali matamshi hayo na kusema hayana msingi wowote.
Kiongozi wa NASA Raila Odinga, katika hatua nyingine amelaani kile anachosema Marekani imeamua kuegemea upande mmoja katika mzozo wa kisiasa nchini humo, na kuitaka iache kuingilia mambo ya nchi hiyo.


Source: RFI

Post a Comment

 
Top