DAR ES SALAAM.
Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 8,157 ikiwemo familia ya msanii wa muziki wa dansi nchini Nguza Viking.
Pamoja na pongezi hizo kituo hicho kimesema kitaendelea kumuomba Rais Magufuli abadili baadhi ya sheria ikiwemo kuondoa sheria inayotoa ruhusa ya adhabu ya kifo.
Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
LHRC imeongeza, “Tunamsihi Mhe. Rais kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta sheria zinazoruhusu uwepo wa adhabu ya kifo na kuifanya hukumu ya kifungo cha maisha kuwa adhabu mbadala”.
Katika msamaha huo Rais pia amemsamehe mzee Mganga Matonya ambaye ana miaka 85 akiwa amekaa gerezani miaka 37 pamoja na miaka saba aliyokaa mahabusu wakati akisubili hukumu yake hivyo kufanya afikishe miaka 44 gerezani.
Kwa hisani ya kusaganews.
Post a Comment