0

PHOTO: Vifaru vikiwa njiani kuelekea Harare.....
HARARE.
Vifaru vinne vimeonekana kuelekea mji mkuu wa Zimbabwe Harare kulingana na watu kadhaa walioshuhudia ikiwa ni siku moja baada ya mkuu wa majeshi  nchini humo Jenerali Constantino Chiwenga kumuonya Rais Robert Mugabe kutoendelea na mpango wa kuwaondoa mashujaa wa vita kutoka chama tawala.

Jenerali Chiwenga amesema "ni lazima ni wakumbushe wanaozusha mvutano wa hivi sasa wa kisiasa kwamba, inapohusiana na kulinda mapinduzi yetu, jeshi halitosita kuingilia kati".

Mapema Jumanne hii Chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Zimbabwe MDC kimetowa wito wa kulinda utawala wa kiraia huku Waziri kivulu wa masuala ya kijeshi wa MDC Gift Chimanikire akisema kwamba "hakuna mtu anayetaka kushuhudia mapinduzi, sidhani kama kuna jaribio la mapinduzi lakini ikiwa jeshi litachukua madaraka, hilo sijambo linalotarajiwa kwani hatua hiyo itafikisha ukomo wa demokrasia nchini mwetu".

Kwa upande wake tawi la vijana la chama tawala cha ZANU-PF kinachomuunga mkono Bi Grace limetowa taarifa na kusema kwamba mkuu huyo wa jeshi Chinwenga hatoruhusiwa kuteuwa viongozi wa Zimbabwe.



Source: VOA

Post a Comment

 
Top