0
MBEYA.
Mkuu wa Mbeya Amosi Makalla amewataka wafanyabishara wa soko la Sido mkoani Mbeya soko liliungua kwa moto na kusababisha mali za wafanyabiashara kuungua ambapo ni mara ya tatu mara baada ya kuamishwa kutoa soko la Mwanjerwa na kuamishiwa katika eneo hilo la Sido.


PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Mbeya aliyenyoosha mkono akielekeza jambo, (kulia kwake) ni Kamishina wa TIRA Dkt Saqwale wakielekea sehemu yalipo majengo ya soko la sido.

PHOTO: Wakikagua sehemu za mabanda ya biashara zilizo tayari na zile ambazo bado kufunguliwa.
PHOTO: Ukaguzi unaendelea.

PHOTO: Akiendelea kukagua huku akiwasalimia wananchi na wafanyabiashara sokoni hapo.


PHOTO: Mara baada ya kuzunguka kukagua mabanda ya biashara yaliyo wanafanya majumuisho kabla ya kuongea na wafanyanbiashara na wananchi.

PHOTO: Dkt. Saqwale akiongea na wafanyabiashara pamoja na wananchi juu ya umuhimu wa kinga ya Bima.


PHOTO: Wananchi wakimsikiliza Dkt. Saqwale (hayupo pichani) 

PHOTO: Dkt. Saqwale akiongea na wafanyabiashara pamoja na wananchi juu ya umuhimu wa kinga ya Bima.

PHOTO: Wananchi wakishangilia kukaribisha Mkuu wa mkoa wa Mbeya jukwaani


PHOTO: Mkuu wa mkoa wambeya Amosi Makalla akiongwa na wafanyabiashara na wananchi.

PHOTO: Wananachi wakirudisha salamu kutoka kwa mkuu wa mkoa wa mbeya (hayupo pichani)

PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiongea na wafanyabiashara na wananchi katika soko la Sido jijini Mbeya



















PHOTO: Mmojwa wa wafanyabiashara Frank Festo ambaye aliunguliwa bidhaa zake akipokea mfano wa hundi ya malipo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya kulia.

PHOTO: Mmojwa wa wafanyabiashara Mohamed O. Magayu ambaye aliunguliwa bidhaa zake akipokea mfano wa hundi ya malipo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya kulia.

PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Mbeya mwenye miwani Amosi Makala (kulia) Mkurugenzi wa TIRA Dkr Saqware wakicheza wimbo wa Kinyakyusa pamoja na wananchi

PHOTO: Picha ya pomoja ya Mawakala na Maneja wa
makampuni ya Bima wa Nyanda za juu kusini mkoani Mbeya.


PICHA ZOTE: Na Leonard Mutani aliyepo Mbeya.



HABARI KWA UNDANI.
Wakati wa kuungua kwa soko hilo baadhi ya wanasiasa walikwenda na wananchi  na ajenda ya kuwepo kwa mbinu za kuamishwa kwa wafanyabiashara wa soko hilo la Sido ambapo baada ya tume iliyoundwa na mkuu wa mkoa Amosi Makalla, ambapo baada ya tume kugundua madhara ya moto eneo hilo yamekuwa yakisababishwa na aina ya majengo yaliyopo eneo hilo, ambayo ni ya mbao.

“Tuliwasiliana na mamlaka za juu, tukaongea na watu wa Sido tukasema tusipofanya maamuzi hapa, soko hili litaendelea kuungua miaka na miaka, tarehe 23 nilikuja kufanya maamuzi hapa ambapo serikali inayoongozwa na Dr. John Magufuri imedhamilia nyie kuendelea kukaa hapa, kama mlijenga kwa mbao inabidi mjenge kwa matofari.” Alisema Amosi Makalla.

Hata hivyo amewaonya madiwani wa jiji la Mbeya kwa kumtupia lawama kutokana na kutengua maboresho ya kubadilisha matumizi ya soko la uhindini na kuwa sehemu ya maegesho ya magari, ambapo katika uchunguzi wake aligundua majina ya madiwani zaidi ya 170 ambao siyo waanga wa eneo husika.

Aliongeza kuwa “nawapa meseji wakae na wale watu wawaeleweshe, wao ndiyo wenye maaamuzi wasililete kwa mkuu wa mkoa, watimize wajibu wao, mimi ni mkuu wa mkoa napingana na maamuzi yasiyo na tija kama ya parking, ikiwa wao ndiyo wenye maamuzi na aridhi ile wanapaswa wawashirikishe wananchi wajue hatma yao, tumewachagua na kuwa amini wasikwepe majukumu yao, wakifanya maamuzi yasiyo ya haki watakuja kulaumiwa baadaye na siyo mbali ni 2020”

Katika mkutano huo kamishina mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) Dr. Saqwale aliyehudhulia mkutano huo ambapo ametoa nasaha kwa mwananchi ambaye ana malalamiko ya Bima afike ofisini ili kuweza kuona kampuni inayofuatilia kero ya mwananchi husika.

“Ni haki yako mwananchi kutambua haki yako kujua maana ya Bima, aina ya Bima kutambua haki yako ndani ya mkataba wa Bima na kujua namna ya kuanzisha shughuli ya Bima, maana Bima ni Biashara, na ninyi mkiwa kama wafanyabiashara mna haki ya kupata elimu ya Bima ili mkiweza muwe mawakala wa Bima”. Alisema Dr. Saqwale.

Wakati majanga yanapotokea na kudumaza uchumi, mara kadhaa wananchi wamekuwa wakirudishwa nyuma kimaendeleo kutokana na hasara inayotokana na janga hilo, mfano wa moto uliotekeza soko la sido mkaoni Mbeya, athari hizo hazi ishii kwa mtu mmoja kama familia bali ni taifa zima.

Aliongeza kuwa “soko linapoungua, biashara zinapotekea kundi la watanzania na taifa kwa ujumla linadumazwa na athali ya moto huo kupitia mnyororo wa thamani, serikali imepata hasara kwa kukosa kodi, wananchi wamekosa ajira, biashara yoyote inayomsaidia mwananchi vilevile inaleta faida kwa serikali kupitia kodi na kutoa ajira. Hivyo wananchi watumia Bima ili kupata thamani mara majanga yanapotokea”


Hata hivyo amelomba jeshi la polisi kupitia serikali ya mkoa kuwadhibiti waalifu wachache wanaouza Bima feki hasa za magari ambazo upelekea wananchi kukosa mafao yao pale wanapopatwa na majanga.

Post a Comment

 
Top