0
KUMEKUWEPO na gumzo kutokana na picha moja ya simba wawili wa kiume walioonekana kwenye mbuga ya maasai Mara nchini Kenya wakifanya tendo la uzinifu ambapo imezuia hisia kali miongoni mwa watu nchini humo na hata katika ukanda wa Afrika mashariki.

PHOTO: Simba walioko katika mbuga ya wanyama nchini kenya
ambao wanasemekana kuwa na mahusiano ya aina moja.
Kufuatia hali hiyo Ofisa wa bodi ya usimamizi wa ubora na udhibiti wa sinema na filamu na viwango nchini humo Ezekiel Mutua amefunguka na kusema kuwa wanyama hao watakuwa wamejifunza tabia hiyo mbaya kutoka kwa binadamu.

PHOTO: Ezekiel Mutua ambaye amejitokeza na
kukemea tabia iliyoonekana kwa simba hao.
Aitha ameongeza kuwa ''simba  hawa wanahitaji kupatiwa ushauri wa kisaikolojia kwa sababu huenda wamekopi tabia hii kwa binadamu wapenzi wa jinsia moja ambao huenda waliwahi kutembelea mbuga hiyo na kufanya matendo ya tabia mbaya mbele ya wanyama hao''.

Afisa huyo ametaka utafiti wa kisayansi kufanyiwa simba hao kubaini chanzo cha wawili hao kushiriki katika tendo kama hilo, amesema kuwa tabia hiyo huenda inatokana na kutawaliwa na mashetani.

''Duniani umewahi kusikia kitendo kama hiki kikitokea?, bali mapepo ambayo huwatawala binadamu sasa tunaona yameanza kuwaingia wanyama, hali hiyo ndiyo sababu ninataka wanyama hao watengwe na watafiti kuchunguza tabia zao iwapo ni za kawaida hama la!'' kauli ya mwisho ya Mutua.


Post a Comment

 
Top