0
Tajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote ambaye pia ni mwekezaji mkubwa hapa nchini ameonya sera za Rais John Pombe Magufuli kuwa  zinawaogopesha wawekezaji.

Profile PHOTO: Tajiri namba moja Afrika Aliko Dangote. 
Dangote ambaye amewekeza dola za kimarekani 650mil kwenye uzalishaji wa saruji, amesema  wakati umefika kwa raisi Magufuli kuzipitia upya sera zake vinginevyo akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote hapa nchini.

Raisi Magufuli alipoingia madarakani, wawekezaji na wafanyabisahara walifurahishwa kwa jinsi alivyopambana na rushwa lakini miaka miwili baadae kufikia sasa, baadhi ya wafanyabiashara wamegubikwa na hofu hasa baada ya kuona mazingira ya kibiashara yamebadilika kutokana na mfumo wake wa utawala.

Mapema mwaka huu rais Magufuli alianzisha uchunguzi wa kina kwenye sekta ya madini na kubaini uhalifu mkubwa ambao ulisababishwa kuundwa kwa sheria mpya ya madini.

Katika kongamano lililofanyika mjini London, mfanyabiashara huyo alisema sheria mpya zinazoundwa zinaiweka nchi kwenye hatari ya kuwafukuza wawekezaji wote na kushindwa kuwarejesha tena.

Kwa sasa Serikali ina amini kwamba sheria hizo zitawanufaisha wananchi kutokana na rasilimali za taifa licha ya kwamba makampuni ya kigeni yamekuwa yakipinga mabadiliko hayo ya sheria kwa madai hazitekelezeki.



Source: BBC

Post a Comment

 
Top