MWANZA.
![]() |
| PHOTO: gari iliyopata ajali. |
Watu wanane wamefariki dunia na wawili kati yao wameokolewa wakiwa salama baada ya gari aina ya Toyota Hiace kutumbukia Ziwa Victoria kwenye kivuko cha Kigongo Feri wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
“Kwa sasa uokoaji unaendelea, ambapo abiria wawili ndiyo wametoka salama na zimeopolewa miili ya watu nane waliokufa,” amesema Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mkoa wa Mwanza, Ferdinand Mshama.
Msimamizi wa kivuko hicho ni Temesa.
Mshama amesema kuwa gari hilo lilikuwa linafanya safari kati ya Buhongwa jijini Mwanza na kivukoni hapo.
Amesema ajali hiyo imetokea kutokana na gari hilo kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki hivyo liligonga geti la kivuko na kutumbukia ziwani.
“Ni kweli gari limetumbukia, lilikuwa likitokea Buhongwa kupeleka abiria kivukoni, kabla dereva hajapaki lilifeli breki,” amesema na kwamba dereva alipita upande wa magari makubwa.
![]() |
| PHOTO: umati wa watu waliokuwepo kandokando ya ziwa Victoria kushuduia tukio hilo. |
![]() |
| PHOTO: Moja ya mwili ulioopolewa kutoka majini. |
Source: Malunde1 Blog.
UPDATE:
kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema kuwa Hiace hiyo ilivuka geti la kwanza na la pili kisha likatumbukia ziwani ambapo mpaka sasa watu wazima walioopolewa ni tisa (9) na watoto watatu (3) ambapo majeruhi ni watano (5)



Post a Comment