0
DAR ES SALAAM 
PHOTO: Sheikh Ponda akiongea na wanahabati
(hawapo pichani) 
Waandishi wa vyombo kadhaa vya habari waliokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na sheikh Ponda Isaa Ponda wamewekwa chini ya ulinzi kwa muda usiopungua dakika 50 toka saa 04:12 mpaka saa 05:02 asubuhi na askari walifika katika ukumbi wa mikutano hoteli ya IRIS iliyopo mtaa Livingston jijini Dar Es Salaam. 

Katika mkutano huo ambao sheikh ponda alikuwa akitoa majumuisho ya safari yake mara baada ya kutoka nchini Kenya kumjulia hali Mbunge ambaye pia ni rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika ambaye amelazwa nchini humo jijini Nairobi baada ya kufyatuliwa risasi zaidi ya 35 na watu wanaosemwa hawajulikani. 

Akiongea mambo kadhaa ambayo miongoni mwa hayo yapo katika ukurasa wa habari za TNEWS kwa njia ya Video (kulia)

PHOTO: Wanahabari wakimsikiliza na kuandika habari kutoka kwa sheikh ponda (mwenye kofia mbele katikati) 

Askari hao walifika hotelini hapo na kuingia huku wakimtafuta sheikh Ponda ambaye kwa wakati huo alikuwa amekwisha ondoka, waliwataka wanahabari kutoondoka mahali hapo pale walipojiridhisha kuwa sheikh Ponda hayupo mahali hapo ndipo walipoondoka huku wakiwashikilia waandishi wawili waliokuwa wakipiga picha tukio lililokuwa likiendelea huko nje kwenye magari mawili waliyokuja nayo askari hao.

Hata hivyo hakuna taarifa za ndani kuwa lengo la askari hao lilikuwa ni nini kufika mahali hapo kwa kumtafuta sheikh huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akitafutwa na hata kushikiliwa na jeshi la polisi nchini kutokana na mambo yanayoonekana ni ya uvunjifu wa Amani.

Habari zaidi alichozungumza sheikh huyo inapatikana kulia kwa ukurasa wetu wa habari za video kulia.



Post a Comment

 
Top