0
Profile PHOTO: Tundu Antipass Lissu

Wakati Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), akitarajiwa kifanyiwa operesheni ya 15 wiki hii, taarifa mpya ambazo gazeti hili limezipata zinadai kuwa Mbunge huyo tayari ameanza mazoezi ya viungo. 

Vyanzo vya uhakika kutoka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikolazwa Lissu kwa zaidi ya siku 40 sasa, vimeliambia MTANZANIA kuwa ndani ya siku nne kuanzia sasa kuna uwezekano mbunge huyo akatoka hospitalini.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu nyumbani kwake mjini Dodoma alipokuwa anahudhuria vikao vya Bunge. 

Vyanzo vya habari vilivyozungumza na gazeti hili jana kwa sharti la kutotajwa majina vilieleza kuwa, awali taarifa za kitabibu zilionyesha kuwa Lissu angetoka hospitali Oktoba 31 mwaka huu, lakini kutokana na hali yake kuimarika anaweza kuruhusiwa kabla ya muda huo.
"Taarifa za kitabibu zilikuwa zinaonyesha kwamba Oktoba 31 mwaka huu, Lissu atoke hospitalini lakini recovering (namna anavyopata nafuu) yake imeonekana haraka. 

"Juzi na jana (Jumamosi na Jumapili), Lissu alianza kutolewa nje akiwa kwenye wheel chair akiota jua... hivyo ndani ya siku nne kuanzia sasa atakuwa ametoka", kilisema chanzo hicho cha habari.

Pamoja na taarifa hizo, haijajulikana endapo mwanasheria huyo mkuu wa Chadema, akitoka hospitalini ataendelea kubaki Kenya au atarudi nyumbani.

Gazeti hili lilipomtafuta Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakujibu. 

Ikumbukwe kuwa msemaji wa suala la Lissu tangu kushambuliwa kwake ni Mbowe, hivyo hakuna kiongozi mwingine wa Chadema aliyekuwa tayari kuzungumzia hali yake. 

Tukiwa tunaenda mtamboni Chadema kupitia msemaji wake Tumaini Makene, alitoa taarifa za kuwa leo watafanya mkutano na wana habari kuzungumzia hali ya mbunge huyo.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top