Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe mwenye miaka 93 ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa balozi wa magonjwa ambukizi ya kifua kikuu na shirika la afya duniani WHO.
PHOTO: Zimbabwe President Robert Mugabe. |
Shirika hilo lenye nguvu katika sekta ya Afya duniani limefuta uteuzi wa rais huyo kama balozi wa nia njema na mustakabali wa WHO.
"Nimesikiliza vizuri wale wote ambao wameelezea hisia zao," kiongozi wa shirika la Afya ambaye ni mwafika wa kwanza Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema katika taarifa yake.
Hapo mwanzo bwana Tendros aliisifu Zimbabwe kwa kujitolea kuboresha afya kwa wananchi wake licha ya Rais Mugabe kwenda kutibiwa nje ya nchi huku akiacha wananchi wake wakiteseka kwa kukosa huduma bora.
Hata hivyo wakosoaji wengi walisema kuwa mifumo ya afya nchini Zimbabwe imeshuka sana chini ya utawala wa Mugabe wa miaka ipatayo 30.
Wafanyakazi mara nyingi wamekuwa hawapati mshahara na hata madawa wakati mwingine hukosekana, bwana Tedros alisema ameongea na serikali ya Zimbabwe na kuamua kumvua Mugabe wadhifa huo.
Post a Comment