DAR ES SALAAM.
Shirika lisilo la
kiserikali la Twaweza limetoa tafiti
inayoangazia utolewaji wa taarifa kwa umma ikionyesha kuwepo kwa ukinzani kwa
maofisa wa serikali kutokuwa na ushirikiano kwa wananchi na wadau wa habari
ikizingatiwa kuwa utolewaji wa habari ni haki kwa kila mwananchi kupata na
kupewa taarifa.
![]() |
PHOTO:
Kajibu Mukajanga akiongea na wanahabari
(hawapo pichani) kuhusu tafiti ya haki ya
kupata habari kwa wananchi.
|
Akikizungumza wakati wa
mjadara huo Kajubi Mukajanga ambaye ni meneja wa Twaweza amesema sheria ya
kutoa taarifa imepiganiwa kwa muda mrefu mpaka kupatikana ila inashangaza kuona
baadhi ya vyombo vya serikali havitoi taarifa “tunaiomba serikali ihakikishe sheria ya
kupata taarifa inafanya kazi, maana sheria hii ndiyo itaweza kumpa nafasi
mwanchi kwenda sehemu yoyote au katika idara yoyote na kutaka apewe taarifa
maendeleo ya watu” alisema
Mukajanga
Sheria hiyo
iliyopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais mwaka mmoja uliopita inaonekana
kutoanza kutumika kwa sababu zisizofahamika, hata hivyo hakuna ofisa yeyote wa
serikali anayeweza kuizuia kufanya kazi kwa kutokutimiza wajibu wake.
Aliongeza kuwa “vinginevyo
itakuwa ni danganya toto hauwezi kuwa na sheria iliyopitishwa na bunge na
kusainiwa na Rais eti haifanyi kazi kwa sababu watendaji flani hawajatimiza
wajibu wao”.
Wakati Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zenye sheria ya kupata
taarifa duniani bado sheria hiyo haijawekwa katika gazeti la serikali ili iweze
kutumika rasmi hivyo kuwakosesha 80% ya watanzania wanaojua wana haki ya kupata
taarifa.
PHOTO:
Meneja utetezi Ananstazia Rugaba akiongea
kuhusu wakati kutoa tathimini kwa vyombo vy habari.
|
Meneja wa mradi huo
Anastazia Rugaba ameiomba serikali kuwashirikisha wadau ili kutengeneza kananu
zitakazosaidia sheria hiyo iweze kuanza kufanya kazi ambapo itatoa nafasi kwa
wananchi kwenda katika ofisi au idara yoyote kupata taarifa.
“kila ofisi ya serikali ina kitengo cha kutoa taarifa lakini
bado maofisa wa hivi vitengo wamekuwa ni wagumu wa kutoa taarifa na wananchi wanaamini kupewa taarifa zozote
isipokuwa zile za usalama wa taifa, na hata wale wenye uwezo wa kutoa taarifa
hawana nyezo, rasilimali za kuwafanya watoe taarifa” amesema Anastazia Rugaba.
Hata hivyo utafiti huo
unaonyesha kuwa katika maombi matatu ya kuomba kupata taarifa ni moja ndilo
lilijibiwa, huku wakipewa muda mrefu wa kupata majibu na baadhi ya idara za
serikali kama taasisi za elimu na vitengo vyake ikiwemo wizara ya Afya haikuwa
raisi kupata taarifa.
Pamoja na hayo ofisi za
Aridhi, Maji na Mipango kwa wastani walijitahidi kutoa taarifa.
Post a Comment