ARUSHA
Hayo yalizungumzwa na Petro Aaron, ambaye ni baba
![]() |
PHOTO: Samson kijana aliyetuhumiwa kwa utekaji. |
Marehemu Samson anatuhumiwa kwa kosa la utekaji na mauaji ya watoto wawili ambaye ni Moureen Njau na Ikhram Salim ambapo aliwaua na kuwatumbukiza katika mtaro wa maji machafu.
Aidha kamanda wa polisi mkoani Arusha , Charles Mkumbo ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa siku ya jumatano iliyopita na kutaka kutoroka ndipo polisi walipoamua kumjeruhi miguu yote miwili.
Kutokana na majeraha hayo, mtuhumiwa alipoteza damu nyingi na kumpelekea mauti kumkuta.
‘’Mtuhumiwa alijaribu kutoroka, ndipo polisi walipolazimika kumjeruhi miguu yote miwili na kukimbizwa hopsitali ya Mkoa Mount Meru akibubujikwa na damu ndipo alipofariki dunia‘’
Tukio hilo lilitokea baada ya mtuhumiwa Samson, kukubali kuonesha eneo alilokuwa akiishi kijana mwingine aliyeshirikiana naye katika kufanya uhalifu huo.
Post a Comment