0
NAIROBI. 
Mahakama ya Juu nchini Kenya imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi uliopita katika uamuzi kuhusu kesi iliwasilishwa na muungano wa upinzani National Super Alliance.


Wakati uchaguzi huo umefutwa na kutarajiwa kufanyika baada ya siku 60, nchi ya Kenya kwa sasa inaingia katika historia ya pekee ikiwa ni pamoja na mahakama ya nchi hiyo kutoa maamuzi kwa kufuata sheria.

YANAYOJIRI NCHINI HUMO KWA SASA. 
Mgombea urais wa upinzani Raila Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika, kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais.
"Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan."

Bw Odinga amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.




MUSYOKA: Heshima ya mahakama imerejeshwa


Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka amesema mahakama imekuwa mfano mwema kwa Afrika na dunia nzima.
"Ninajivunia kuwa Mkenya leo," amesema.
"Sasa tutaangalia kwa kina kuhusu tume ya uchaguzi. hatuna imani kwamba wanaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki."

PICHA CHINI: wafuasi walio upande wa Raila Odinga mjini Kisumu wakishangilia kufutwa kwa matokeo ya Urais.






Kusherehekea ushindi wa Odinga Nairobi


PICHA CHINI: Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga jijini Nairobi wamekuwa barabarani wakisherehekea hatua ya mahakama kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais.



PICHA CHINI: Nje ya mahakama  ulinzi mkali umewekwa na umendelea kuwepo hata sasa jijini Nairobi.





Source: BBC

Post a Comment

 
Top