 |
PHOTO: Aliyesimama: Godfrey Edward Afisa biashara Arusha, kulia kwake kwake ni Mwenyekiti wa Wanjamuco Alex Lasiki. |
ARUSHA.
Chama cha wauza nyama
mkoa wa Arusha (WANJAMUCO) kimefanya
sherehe ya kutimiza mwaka mmoja, akizungumza katika sherehe sherehe hiyo Afisa biashara
wa mkoa Godfrey Edward aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa wilaya ya
Arusha amesema, wakati ushindani wa biashara ya ng’ombe unazidi kuwa mkubwa na
ng’ombe wengine wakisafirishwa nje ya nchi, serikali imekuwa inakosa mapato
kutokana na kuwepo kwa madalali.
 |
PHOTO: Baadhi ya wanachama wa wanaounda umoja wa wauza nyama jijini Arusha (WANJAMUCO) wakimsiliza Afisa biashara wa mkoa Geofrey alipokuwa akitoa hotuba. |
 |
PHOTO: Picha ya pamoja wanachama wakiwa na viongozi wao mara baada ya sherehe nya kutimiza mwaka mmoja |
HABARI KWA UNDANI.
Ameongeza kuwa
Wanjamuco hao kuboresha umoja wao na kuweza kuthibiti biashara holela ya bucha
za nyama ambazo zinazagaa mtaani na sehemu ambazo zisizofaa kuwekwa maduka ya
nyama, “tukiwa
na nia moja kwa kuweka mbele utoaji wa huduma bora na ushirikiano tutaweza
kuthibiti mabucha yaliyo chini ya viwango”
alisema Godfrey.
Wakati nchi ikiwa inaelekea
katika uchimi wa viwanda, wauzaji hao wa nyama wameitaka serikali kuzuia
uuzwaji wa mifugo nje ya nchi ili kuweka nafasi ya mazao gafi zitokanazo na
mifugo kama ngozi, maziwa, pembe,kwato vizalishwe hapa nchini na kutumwa nje ya
nchi kama bidhaa nyingine ili kukuza mapato na ajira nchini.
Naye mwenyekiti wa
umoja huo Alex Lasiki amesema pamoja na changamoto nyingi zinazowakumba wauzaji wa
nyama bado wanaiomba serikali kuweka mikakati itakayoweza kupata kodi kutoka
kwa madalali wa mifugo wanaopata mapato kutokana na mifugo isiyo kuwa yao na
ndiyo wanaosababisha kupanda kwa bei ya mifugo.
“tunaiomba serikali ituunge mkono kupiga vita biashara holela ya
wauza nyama wanaokuja kwa msimu wanaosababisha tasnia ya nyama hasa
tunazopeleka nje inaonekana haina kiwango, kwani nyama ni bidhaa ambayo
ukiitumia vibaya inaweza kukudhuru” alisema Lasiki.
Pia wameiomba mamlaka
ya mapato nchini TRA kutoa elimu juu yam ashine za kukusanyia kodi Efds ili kuweza
kuepusha migangano inayoweza kujitokeza kutokana na ununuzi, uuzaji na
upatikanaji wa mapato kwa wauzaji wa nyama mkoani Arusha.
Umoja huo wenye jumla
ya wanachama 112 unawaunganisha wauzaji wa nyama mkoani Arusha ambapo kati ya
hao 100 ndiyo walio hai katika kuchangia na kuhudhulia katika mikutano na
shuguli mbalimbali za umoja huo.
Hata hivyo serikali
imekuwa mstali wa mbele katika kuboresha na kuandaa mazingira mazuri ya usafirishwaji
wa mifugo pamoja na mazao yatokanayo na mifugo ili kusafirshwa nje ya nchi ili
kuweza kulinda mapato ya wafugaji, wanunuzi na wauzaji wa ndani.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.