PHOTO: Jaji
wa mahakama ya kimataifa
ya makosa ya jinai ICC Bertram
Schmitt |
BILA SHERIA HAKUNA KOSA,
Warsha
ya mafunzo ya kimataifa juu ya sheria na makosa inawakutanisha wadau mbalimbali
kutoka nchi kadhaa duniani ikiwa ni katika kupambana na uhalifu wa kwenye
nyanja za kimataifa na wakimataifa katika mradi wa Afrika mashariki ukiwa chini
ya usimamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani.
PHOTO: Jaji
wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC
Bertram Schmitt, aliyesimama akiwasilisha mada kuhusu
uwezeshaji
Katika mahakama pamoja na mapungufu kwa upande wa fedha (bajeti)
|
PHOTO
JUU NA CHINI: Wahudhuliaji kutoka taasisi mbalimbali za
kimahakama kama wanasheria, majaji na mawakili wakifuatilia mada.
PHOTO: Mwandishi
wa habari hii Leonard Mutani (kulia) akifanya mahojiano na Wakili wa kujitegemea Nelson Ndeki kuhusu
umuhimu
wa kongamano hilo.
|
ARUSHA.
Katika warsha hiyo ya wataalam
maarufu na wataalam wa kuongoza mradi wa
Wayamo iliyojumuisha nchi nyingi za Afrika wakiwemo mawakili, majaji kutoka
nchi za Afrika mashariki ikiwemo Tanzania imeanza leo jijini Arusha.
Jaji wa mahakama kuu
nchini Jaji Othuman Chande amesema mkutano huo wenye lengo la kuzungumzia uhuru
wa mahakama, utawala wa kisheria, utendaji wa mahakama za kimataifa na uhusiano
wake na makosa ya jinai ambayo yanayofanyika nje ya mipaka ya nchi ambako makosa
yanafanyika kimataifa.
Ameongeza kuwa “usafirishaji binadamu,
kuua wanyamapori, ni moja kati ya makosa
yanayofanyika kimataifa na vita yake siyo ifanyike hapa Tanzania lakini pia
hata nje ya mipaka” hivyo ametoa
wito kwa vyombo vya dola kutoa ushirikiano katika nchi zinazo athirika na janga
hilo.
Aitha warsha hiyo
imewakutanisha majaji maarufu kutoka mahakama ya kuu ya makosa ya Jinai The Hague
mstaafu Navil Pillay, Jaji wa mahakama ya juu ya nchini Marekani Jaji Sonia
Sotomayor na Rais wa zamani wa mahakama ya Rwanda Jaji Muyoboke Karimuda na
majaji wa Afrika Mashariki hata wanasheria wakujitegemea akiwemo Nelson Ndeki
kutoka Tanzania.
>>>HABARI KAMILI INGIA KATIKA HABARI VIDEO KULIA KWA UKURASA WETU.
Post a Comment