ARUSHA.
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu
la Arusha, limetoa kauli kwa nini limekataa kuendesha misa ya maziko ya
mfanyabiashara bilionea Faustine Mrema kwa madai hakuwa na Sakramenti ya ndoa
na mke wake wala kipaimara.
PHOTO: Marehemu Faustine
Mrema.
|
Paroko Msaidizi wa
Parokia ya Mtakatifu Theresia, Mtoto Yesu, Jimbo Kuu la Arusha Padri Festus
Mangwangi amekiri suala hilo na kuongeza kuwa marehemu enzi za uhai wake
hakuweka heshima na kanisa.
“Marehemu ni mkatoliki wa kuzaliwa, lakini hakuwahi kuwa na
sakramenti ya ndoa na mke aliyezaa naye watoto wala kupata Kipaimara. Kanisa
haliwezi kumzika kabisa, kawaida mazishi ya Kanisa Katoliki ni heshima
inayotolewa kwa mhusika kama anastahili” alisema Padri Mangwangi
Aliongeza kuwa “Huyu hakuwahi kufunga ndoa kanisani, alijitenga na kanisa
kwa hiyo kusema tumemtenga si kweli, yeye ndiyo alijikataa hakutaka kutafuta
heshima yake na kanisa akiwa hai.”
Kuhusu kutokwenda kwenye
Misa za Jumuiya ambayo nayo ni moja ya taratibu muhimu inayowataka waumini wa
kikatoliki kushiriki ibada za nyumba kwa nyumba Padri Mangwangi amesema, hata
ibada hizo nazo pia marehemu alikuwa hashiriki.
“Jumuiya ni utaratibu wa kanisa unaowataka waumini wawe na
ushirika wa karibu ikiwamo kufahamiana marehemu pia alikuwa hashiriki kabisa
sasa unaanzaje kumzika mtu kwa heshima za Kanisa Katoliki?” amehoji Padri
Mangwangi.
Wakati Kanisa hilo
likijivua kushiriki Misa ya heshima ya maziko ya marehemu Mrema hiyo jana,
Askofu Dk. Eliud Issangya wa Kanisa la Kimataifa la Kiinjili, alilazimika
kuongoza Ibada hiyo ya maziko iliyofanyika Hoteli ya Ngurdoto, wilayani Arumeru.
Source: Mtanzania.
Post a Comment