ARUSHA.
Benki ya NMB nchini inawakutanisha wafanyabiashara ambao
ni wateja na wasio wateja wa benki hiyo kupitia vyama vijulikanavyo kama CLUB
zilizopo katika kanda maalum ikiwa ni katika kuwapa elimu na kusikiliza
matatizo, kero na mapungufu yaliyopo wakati wa hutoaji huduma kwa wateja wa
benki hiyo.
PHOTO: Meneja wa NMB Kanda ya kasikazini
Salie Mlay akiongea hadhima ya semina hiyo wakati wa kumkaribisha mgeni.
|
PHOTO:
Baadhi ya wanachana
na wadau waliofika kupata elimu na kuuliza kwa undani juu ya huduma mbalimbali
za benki ya NMB.
|
PHOTO: Afisa tawala wa mkoa wa Arusha Polycarp
Kuyumba aliyeshika kipaza sauti alimwakilisha mkuu wa mkoa katika ufunguzi wa semina ya NMB Club
iliyofanyika jijini Arusha mapema leo.
|
PHOTO: Wadau wa klabu ya Nmb Arusha wakimsiliza Afisa tawala alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo. |
HABARI KWA UNDANI....
Katika ufunguzi wa
semina kwa wanachama wa Benki hiyo kanda ya kaskazini iliyofanyika jijini
Arusha, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Afisa Tawala wilaya ya Arusha Polycarp
Kayumba amepongeza juhudi kubwa zilizofanywa na Benki hiyo kwa kutatua kero
nyingi zilizokuwepo kwa wateja wanapokuwa wakitaka mikopo pamoja, kuboresha mapato na kufanya ulipaji wa kodi
kuwa rafiki tofauti na hapo nyuma.
“kwa sasa tunaona Benki imejipanga hata Serikali imeweza kuitumia kwa asilimia
kubwa tofauti na wakati uliopita hii inaonyesha malengo ya serikali inayoongozwa
na Rais John Pombe Magufuri kuiamani na hivyo kuamua kuitumia ukizingatia hii ni
Benki ya Serikali” Alisema
Polycarp Kayumba.
Hata hivyo Nmb imeamua
kujikita kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni katika kuwa na mahusiano kwa
wanachama, Mamlaka ya mapato kwa mkoa wa Arusha, kwa ujumla ambapo utaratibu
huo unanufaisha watu wote kikanda na kitaifa.
Habari zaidi tembelea
ukurasa wetu wa HABARI KATIKA VIDEO
kulia kwako….
Post a Comment