0
DAR ES SALAAM
PHOTO: Mwenyekiti wa CHAWATA nchini (mwenye kofia) John Mlabu
akiongea na wanahabari hawapo pichani kuhusu bajaj ziachwe
na ziendeshwe na welemavu tu pekee. 
Chama cha walemavu nchini CHAWATA,  kimeiomba serikali inayiongozwa na Rais John Pombe Magufuri kuwapa nafasi stahiki pamoja na kuwapa nafasi katika fulsa zinazojitokeza ili waweze kutumika katika ujenzi wa taifa na maendekeo ya taifa kwa ujumla. 

Akiongea na wanahabari leo, mwenyekiti wa chama CHAWATA nchini John Mlabu amesema, jamii ya watu wenye ulemavu wamekuwa wakipata shaka katika mipango kuelekea nchi yenye uchumi wa kati na sera ya kuanzishwa viwanda.

"watu wenye ulemavu tunapata shaka kushiriki katika mipango hii kwani tumekuwa tukiachwa nyuma watu wenye ulemavu kila fuksa zinazojitokeza kundi letu linabaki nyuma kwa muda mrefu kwenye nyanja za kielimu, uchumi, siasa, utamaduni na kijamii" alisema John Mlabu.

PHOTO: Viongozi na wanachama wa chawata walioongozana kuongea  na wanahabari mapema leo jinini Dar Es Salaam. 

Hata hivyo chama hicho kimempongeza Rais John Magufuri kwa mipango ya kuiweka nchi katika uchumi wa kati na viwanda, pia kuwajali watu wa kipato cha chini wakiwemo maskini katika taifa hili.

Vilevile wamemtaka Rais JPM wakati anawatetea Wamachinga na Bodaboda na kuwaacha watu wenye ulemavu watabaki kuwa ombaomba mitaani,  aliongeza kuwa "hii haitapunguzi mawazo tuliyonayo baadhi ya watu wenye ulemavu kukimbilia Dar Es Salaam na majiji mengine tukiamini ndipo kwenye nafuu ya maisha"

Vinginevyo kutokana na usafiri wa bajaj kuwa maalum kwa matumizi ya walemavu wameiomba serikali kuondoa kodi kwa vyombo ivyo ikiwepo serikali kuagiza na kutoa kwa mkopo kwa walengwa wakiwemo umoja wa waendesha bajaj mkoa wa Dar Es Salaam ambao watazitawanya nchini kwa walengwa ambao ni wanachama wao.

Post a Comment

 
Top