0
DAR ES SALAAM
Jiji la Dar es Salaam limeibuka mshindi wa 28 wa tuzo za msafirishaji bora duniani, huku ikiwa nchi pekee kutoka Afrika kushinda tuzo hiyo.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa upanuzi wa lango kuu la Bandari ya Dar es Salaam.
Nikupe hongera wewe Mheshimiwa Rais na serikali yako, kwa sababu jiji la Dar es Salaam limeteuliwa kuwa mshndi wa 28 wa tuzo ya msafirishaji wa dunia,” amesema Bella.

Bella aliongeza kuwa “Ushindi huo ni kupitia mradi wa UDA-RT (mabasi ya mwendo wa haraka), kwa hiyo napenda nikupongeze katika hilo”.
Bella pia amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katikia kuboresha miundombinu na huduma za usafiri nchini na kuahidi kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali kuendelea kuboresha miundombinu na huduma mbalimbali.

Post a Comment

 
Top