PROFILE PHOTO: Zitto Zuberi Kabwe -Kiongozi ACT. |
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, mwenyekiti huyo wa chama cha upinzani, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Said Meck Sadiki.
Baada ya kukaa kimya kufuatia uteuzi huo hatimaye Jumapili hii ya June 4,2017 Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametoa ujumbe ufuatayo: "Nimekuwa naulizwa sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya habari".
Pia aliongeza kwa kusema kuwa "Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana naye, ila tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea nchini".
Hata hivyo amewataka wanachama wote wa ACT wazalendo kuwa watulivu na endapo kutakuwa na taarifa tofauti na masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama watatoa taarifa za kuwajulisha.
Post a Comment