PROFILE PHOTO: Rais John P. Magufuri. |
Baada ya uteuzi na kuapishwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo nchini Anna Mgwira, kuna kile kinachoelezwa kuwa ni ukosoaji wenye faida umeonekana kwa kiongozi huyo wa chama cha upinzani na kuelezwa kuwa Rais bado ana nafasi kuwateua wale wanaomkosoa kwa hoja na si vinginevyo.
Hatua hiyo inatajwa kumuweka Rais Magufuri katika taswira ya kukanganya zaidi kwa kuwa tayari amepata kutoa kauli zinazokandamiza siasa za upinzani nchini, ikizingatiwa kuwa mnamo mwezi juni mwaka jana, alitangaza kusitisha mikutano yote ya kisiasa akitoa ruksa kwa wabunge pekee hali iliyozua malumbano kati yake na viongozi wa vyama vya upinzani.
PHOTO: RC anna Mghwira mara baada ya kuapishwa. |
Katika taarifa iliyopatikana na mmoja wa wandani wa ikulu jijini Dar Es Salaam kwamba uteuzi hio si wa mwisho na kwamba Rais Magufiri haamini kwamba kuna watu wameumbwa kuwa wapinzani maisha yao yote.
"nenda kawaambie Watanzania kwamba Mghwira amechaguliwa kwa sababu ya ukosoaji wenye hoja, hivyo Rais hana shida na wakosoaji wa namna hiyo na siku zote wana nafsi kwa serikali yake," alisema mtoa habari huyo.
Hata hivyo hii ni mara ya kwanza kwa mmoja wa wandani wa Rais Magufuri kuelezea kwa kinaga ubaga kuhusu uteuzi huo wa Mghwira, ambahe alikuwa mshindani wa mgombea wa huyo wa urais wa chama cha mapinduzi ccm kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
Kwa upande mwingine, mtoa habari huyo alisema, "Sasa kuna wakosoaji wengine kila siku wanakosoa tu na wakati mwingine wanaweka matusi na kashfa humohumo, watu kama hawa Rajs Magufuri hawezi kufanya nao kazi"
Aitha kwa tafsiri ya Magufuri, hakuna mpinzani wa kudumu, yeye anaamini vyama visivyo madarakani ni vyama mbadala tu kwa CCM na haimaanishi kazi yao ni kupinga tu bila hoja.
Ujumbe kwa wanasiasa wote ni kwamba yeye (Rais) hana ubaguzi na yupo tayari kufanya kazi na wote wenye hoja.
Source: Raia Mwema
Post a Comment