TODAYS NEWS Tunakumetea dodoso chache kwa yale yaliyonili katika hotuba ya Waziri wa fedha na mipango Mh. Dkr Philip I. Mpango (MB) alipowasilisha bungeni taarifa ya hali uchumi kwa 2016 na mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/18*
>>Kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka 2016,ilikuwa asilimia 3.1 ikilinganishwa na asilimia 3.2 mwaka 2015-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Mfumuko wa bei duniani uliongezeka kufikia wastani wa asilimia 2.9 mwaka 2016 ikilinganishwa na asilimia 2.8 mwaka 2015-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Pato la Taifa lilikuwa kwa wastani wa asilimia 7.0 kwa mwaka 2016-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Pato la Taifa kwa mwaka 2016 lilifikia Shilingi milioni 103,744,606-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Wastani wa pato la kila mtu limefikia Shilingi 2,131,299 ikilinganishwa na wastani wa Shilingi 1,918,897 mwaka 2015-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Mwaka 2016 mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 5.6 mwaka 2015-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Tanzania ni nchi ya tano kwa idadi ya watu Barani Afrika-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi wa Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam-Morogoro(Km 205)-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali imenunua ndege mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja-Dr. Philip Mpango
>>Serikali imesaini mkataba wa makubaliano ya awali ya ujenzi wa Bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda-Bandari ya Tanga-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Ujenzi wa meli mbili za mizigo ziwa Nyasa umekamilika-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Shilingi Billioni 2 zimewekwa kwa ajili ya uanzishwaji wa Shamba la Miwa na Kiwanda cha Sukari Mkulanzi-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Mkoa wa Pwani una jumla ya miradi mipya ya viwanda 82-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Mapato ya kodi kufikia asilimia 14.2 ya Pato la Taifa mwaka 2017/18-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali kufufua kiwanda cha sukari katika Gereza la Mbigiri Dakawa-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali kufufua kiwanda cha kutengeneza viatu katika Gereza la Karanga Moshi-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali kufufua kiwanda cha nguo cha Urafiki-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali kufufua kiwanda cha Morogoro Canvas Mill-Mhe.Dr. Philip Mpango
>>Serikali kufufua kiwanda cha chai cha Mponde kilichopo Lushoto,Tanga-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali kufufua kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali kufufua kiwanda cha Kubangua Korosho cha Tandahimba na Newala-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali kuanzisha viwanda vipya vya Dawa,vifaa vya hospitali na gesi ya oksijeni na kiwanda cha kusindika zabibu Chinangali Dodoma-Mhe. Dr. Philip Mpango
>>Serikali kuanzisha kiwanda cha kuzalisha wanga kutokana na zao la muhogo na viazi vitamu huko Lindi-Mhe. Dr. Philip Mpango.
Prepared by: Habari Maelezo.
Post a Comment