PHOTO COURTESY VOA: Jengo lililoporomoka. |
Kufikia jioni hii, takriban watu 15 hawajulikana walipo kufuatia mkasa huo wa kuporomoka kwa jengo.
Shirika la msalaba mwekundu nchini humo, limesema kupitia ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuwa makundi ya uokoaji yalikuwa kwenye eneo la tukio ili kuweza kutoa msaada.
Mashahidi wameiambia walioshuhudia tukio hilo wamesema kwamba magari ya msalaba mwekundu na magari ya wagonjwa kadhaa zilionekana zikisafirisha watu kutoka eneo la tukio hilo.
Halmashauri ya kupambana na majanga ilisema Jumanne kwamba baadhi ya wakazi walikuwa wametoroka baada ya kuonywa kwamba jengo hilo lilikuwa kwenye hatari ya kuporomoka.
Mnamo mwezi Aprili mwaka huu, takriban watu 49 walikufa baada ya jengo jingine kuporomoka mjini Nairobi.
Source: VOA
Post a Comment