PHOTO: Meli ya Marekani iliyobeba shehena ya vifaa vya kivita kuelekea Korea Kusini. |
Korea Kaskazini inadai kuwa serikali ya Marekani pamoja na Korea Kusini zinapanga mpango wa kumuua kiongozi wao wan chi hiyo Kim Jong-un.
Wizara ya maswala ya usalama nchini ya nchi hiyo imesema mataifa
hayo mawili yanatumia kundi la kigaidi linalosaidiwa na shirika la ujasusi la
CIA na wamepanga mpango huo.
Aidha, Pyongyang inasema mataifa hayo yanapanga kutumia silaha za
kibiolojia kumwangamiza kiongozi huyo machachari anayeitikisa Marekani kwa sasa
kutokana nan chi yake kuamua kufanya majaribio mbalimbali ya siraha hatari za
nyuklia.
PHOTO: Kiongozi wa korea kaskazini Kim
Jong
|
Hata hivyo, Korea Kaskazini imesema itahakikisha kuwa inakabiliana
na kundi hilo la kigaidi, wakati madai haya yameendelea kuzua hali ya wasiwasi
katika eneo la Korea, hata hivyo Marekani na Korea Kaskazini wameendelea
kushambuliana kwa maneno huku wakitishiana kwa kushambuliana kwa makombora.
Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akisema kuwa anaweza
kukabiliana na Korea Kaskazini hata bila msaada wa China kuhakikisha kuwa
haiendelei na mpango wake wa kujaribu silaha za Nyuklia.
Source:
fri
Post a Comment