DODOMA.
Mkutano wa mwaka wa
mashauriano wa Bodi ya usajili wa makandarasi nchini ulioanza jana kwa
kufunguliwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama
Samia Suruhu umehitimishwa leo mjini Dodoma ambapo kauli mbiu inayotumika kwa
mwaka huu ni ‘miaka 20 ya crb, utendaji wa
makandarasi unaozingatia maadili na sheria kama mkakati wa kuaminiwa na waajili’.
PHOTO: Mwenyekiti
wa Bodi ya Usajili wa makandarasi nchini Consolata Ngimbwa akiongea wakati wa
kumkaribishwa Katibu mkuu wizara ya Ujenzi mjini Dodoma katika mkutano wa
mashauliano.
|
PHOTO: Baadhi wa
washiriki wa mkutano huo kutoka nchini wakimsikiliza Mwenyekiti wao Mama
Ngimbwa (hayupo pichani)
|
PHOTO: Naibu waziri wa ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akitoa cheti kwa mmoja wa washiriki wa mkutano wa makandarasi kwa niaba wa weingine 1200 walipota vyeti vya kuhudhuliwa mkutano huo |
KWA UNDANI
Akifunga mkutano huo
ulioudhuliwa na washiriki wapatao 1208 Katibu mkuu wizara ya ujenzi Mwandisi
Joseph Nyamuhanga kwa niaba ya waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbalawa amesema,
wizara ya ujenzi inafarijika kuona bodi hiyo ikifanya mkutano kama huo wenye
lengo la mashauliano kutokana na ukandarasi ni moja kati ya sekta nyeti kwa
kukuza uchumi wa nchi.
Vile vile ameongeza
kuwa pamoja na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa makandarasi kutokupata kazi
moja kwa moja kutoka serikalini, serikali ya awamu ya tano iliyopo chini ya
Rais John Pombe Magufuri inaelewa kilio hicho na inayafanyia kazi.
“kwa kuwa makandarasi walilia na hali ya kutokupata kazi itakuwa
ni wakati muafaka kwa makandarasi kujitathimini kwa mapungufu machache waliyo
nayo ili kuipa serikali yao nafasi ya kuwaamini zaidi, maana kauli mbiu ya mwaka
huu naamini inawapatia hamasa” Alisema Nyamuhanga.
Aliongeza kuwa “Wizara ya
ujenzi, uchukuzi na mawasiliano itaendelea kusimamia kikamilifu sheria ya
ununuzi wa umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013, ili kuhakikisha
miradi yote ya ujenzi wa miundombinu yenye thamini ya shs 8bilioni inayosimamiwa
mfuko wa barabara inakwenda kwa makandarasi wa ndani”
Pamoja na hayo
mwenyekiti wa Bodi ya Usajiri wa Makandarasi nchini Mama Consolata Ngimbwa
amesema katika mkutano huo wamefikia maazimio ambayo watayakusanya na
kuyapelekwa serikalini, ikiwa ni kutokana na maagizo yaliyotokana na kauli ya
makamu wa Rais kuataka wafanye hivyo.
Pia amesema kuwepo kwa
itilifu za kutokuzingatiwa kwa sheria ya ununuzi wa Umma PPA ambapo ameomba sheria
hiyo izingatiwe ili zabuni zitangazwe ili kutoa nafasi kwa makandarasi wote waliosajiliwa
na bodi waweze kushindanishwa.
“Tunaomba mamlaka za ununuzi izingatie kwa kutozitangaza zabuni
mpaka ziwe na uhakika wa makubaliano ya utekelezaji wa yaliyofikiwa” alisema Ngimbwa.
Mkutano huo umefungwa
ambapo umejumuisha makandarasi, waajili, watoa kazi wakubwa, viongozi wa
taasisi mbalimbali, wafadhiri na wafanyabiashara wa bidhaa na huduma mbali
mbali za ujenzi, wakiwemo washiriki kutoka nje ya Tanzania kama Kenya, Malawi
na Zamba.
Post a Comment