Waziri Mwijage Akizungumza katika halfa ya ufunguzi wa duka kubwa la vifaa vya ujenzi
Balozi wa china Tanzania dkt LU Youqing akizungumza katika unguzi wa duka hilo
Bidhaa zinzazopatikana katika duka hilo
Wazri Mwigaje akisikiliza maelekezo kutoka kwa moja wa viongozi wa duka hilo
Waziri Mwijage akitoka katika duka hilo mara baada ya ukaguzi
Wazri Mwigaje akikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa duka hilo.
Waziri wa viwanda na biashara Mhe Charles Mwijage amefungua rasmi jengo la kampuni ya Taifa ya vifaa vya ujenzi la China National Building Material Group Limited (CNBM) lililopo mikocheni jijini Dar es salaam.
Akizungumza hafla ya ufunguzi huo mhe Mwijage alisema kampuni hiyo ni ya kimataifa na yenye viwango imejenga zaidi ya asilimia 65 ya viwanda vyote vya saruji na vioo duniani.
Aliongeza kuwa kampuni ya CNBM ina uwezo mkubwa katika uzalishaji wa cement na imekuwa ikizalisha tani 530 milioni kwa mwaka wakati uwezo wa Tanzania katika viwanda vilivyosimikwa ni tani milioni 10.8 na kubainisha kuwa kiasi kinachohitajika nchini ni tani milioni 4.8.
Pia amesema CNBM inatarajiwa kushirikiana na mwekezaji mwingine ambaye anakwenda kujenga kiwanda Tanga kitakachozalisha tani milioni saba za cement na kubainisha kuwa hakuna kiwanda kinachozalisha tani milioni saba Tanzania.
Aidha mhe Mwijage aliongeza kuwa CNBM kwa kutambua umuhimu wa uwekezaji na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi hapa wamekuwa wakitoa maelekezo kwa wataalam nchini badala ya kununua vifaa hivyo nje ya nchi.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. alisema urafiki baina ya China na Tanzania ni wa kihistoria tangu kwa Rais Xi Jinping ambapo urafiki huo umekuwa mwendelezo hadi kwa serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli.
Nae Mkurugenzi wa China National Building Material Group Limited (CNMB) Bw. Andy Chen amesema kampuni hiyo inatoa fursa ya kazi kwa watanzania pamoja na kutoa mafunzo yatakayowasaidia kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda.
Post a Comment