PHOTO: Seif Hamad, katibu mkuu wa CUF. |
Akiongea katika kituo cha Luninga cha Clouds TV katika kipindi cha 360 katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF amesema kutokana na tatizo la kiuongozi lililopo ndani ya chama hicho ambapo mtifuano uliopo kwa sasa kati yake na Profesa Lipumba amesema "nikimuona Lipumba hata sasa naondoka" kauli hiyo inakuja kutokana na mtifuano huo na hali harisi.
Kwa upande mwingine amesema hawezi kumsamehe Lipunba kutokana na kuwa mtu aliyetumwa kuvunja chama na kuketa mvurugano, hivyo haoni tija katika nafasi yake kuweza kumsamehe.
Hata hivyo amempongeza Rais magufuri kwa kazi nzuri katika awamu yake ya uongozi lakini amemtaka kuboresha masuala ya haki na kuondoa penye uzio kwa wananchi.
Akizungunzia Uhuru wa vyombo vya habari amesema, vyombo vya habari bado vinaminywa na hakuna haki katika mazingira ya wanahabari kupewa nafasi ya kujitetea ila sheria imepitishwa basi.
Post a Comment