0
Mafunzo yaliyoshirikisha walimu wa shule za msingi nchini katika kuwawezesha walimu kuutambua na kuutumia mtaala mpya wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu KKK yaliyoendeshwa katika kanda kadhaa nchini yamefungwa rasmi katika Chuo cha ualimu Bustani kilichopo wilaya ya Kondoa mkoa, Dodoma ikiwa ni moja ya kituo kilichokuwa kikitoa mafunzo hayo ya kwa kanda ya kati.


<<< PHOTO: Hii ndiyo Elimu ya Mtaala Ulioboleshwa jinsi utakavyofundishwa ka KUCHOPEKA, na hii ni Mmoja ya kazi nzuri iliyofanywa na Mwalimu Fredirick Shekiego kutoka Kongwa ni kuunda mfano wa Satelaiti Dishi.



PHOTO: Waziri Suleiman Jaffo akipokea taarifa za awali kutoka kwa Mratibu wa mafunzo wa kituo cha mafunzo ya Mtaala Ulioboreshwa Lucas Mzelela Kulia.


PHOTO: Kutoka kushoto ni Dr. Siston Masanja, DC Makota, Mh. Suleiman Jaffo, Mratibu Lucas Mzelela na Mkuu w Chuo cha Bustani wakielekea katika ukumbi kwa ajili ya kuhitimisha mafunzo.

PHOTO: Dr. Siston Masanja Mtendaji mkuu wa ADEM akiongea wakati wa shuguli ya kufunga mafunzo, (kulia kwake) ni Lucas Mzelela na (Kushoto) Mh. Jaffo wakimsikiliza.

PHOTO: Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota  akiongea wakati akaimkaribisha Waziri Jaffo kuongea na walimu kisha kuhitimisha mafunzo ya Mtaala mpya wa KKK.

PHOTO: Waziri  katika ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo akiongea na walimu (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo na jinsi serikali ilivyojitoa kufanikisha mafunzo ili kufikia Elimu bora kwa watoto nchini.

PHOTO: Walimu, wakufunzi na washiriki wa mafunzo ya Mtaala Ulioboreshwa wakimsikiliza mgeni Rasmi Mh. Jaffo hayupo pichani wakati akitoa hotuba ya kufunga mafunzo.

PHOTO: Picha ya pamoja viongozi wa ADEM, Mkuu wa wilaya ya Kondoa, Maafisa Elimu wa wilaya za mkoa wa Dodoma, wakufunzi mbalimbali na Mgeni rasmi Mh. Suleiman Jaffo katika kumbukumbu ya pamoja.


KONDOA DODOMA.
Akitoa taarifa za kuhitimisha mafunzo hayo, Mratibu wa mafunzo wa kituo cha Bustani Lucas Mzelela amesema mafunzo hayo yamesimamiwa na ADEM ikishirikiana na Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania, wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambapo wahitimu wamepewa mafunzo yaliyoambatana na itihali kuweza kuwafanya wananfunzi kuepa katika masomo yao.

“Washiriki wamepitishwa kujenga umahili katika maeneo kadhaa kama kuchambua mtaala ulioboreshwa wa 2016, kuchambua mutasari wa darasa la 3 na 4, miongozo ya kufundishia, maandalizi ya ufundishaji na kuchambua mbinu stahiki za ufundishaji zinazoshirikisha wanafunzi katika ufundishaji lakini pia wameweza kufundisha kidogo kuhusu KUCHOPEKA kupiti stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa wanafunzi wa darasa la 3 na 4.” amesema Lucas Mzelela.
Vilevile Mtendaji mkuu wa ADEM Dr. Siston Masanja ameishukuru serikali kwa kuweza kuwaamini na kuwakabidhi jukumu la kusimamia mafunzo hayo ambapo amesema wakufunzi kutoka vyuo vya elimu ambao wamehudhulia mafunzo hayo watakuwa ni chachu ya stadi ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu ianze kufundishwa na kupata walimu wenye weledi kwa siku za usoni.
Hata hivyo amesema wahitimu hao wana deni kubwa mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo na hategemei kuwepo kwa kisingizio kutokana na maarifa, uwezo wa kupambana na changamoto za kawaida ambazo zinawakabili kupitia shule wanazofundisha.

“Itakapofika mwaka 2050 kutakuwa na watoto milioni 300 wasiojua kusoma, kuandika na Kuhesabu, hivyo basi sisi kwa mafunzo haya na yanayoendelea tuseme tutachangia  watoto 0% maana serikali inatoa fedha nyingi.” Amesema Dr. Siston Masanja.

Mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo naibu waziri katika ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo kwa niaba ya serikali amewapongeza wasimamizi wa mafunzo kwa kufanya mafunzo hayo kuwa rafiki na uratibu wa mafunzo hayo umewezesha katika mipango ya serikali kuonyesha mwanga katika sekta Elimu kupitia usimamizi wa ADEM.

Pamoja na washiriki wote waliokusudiwa kuhudhulia mafunzo hayo kuhudhuli kwa asilimia 100, nafasi ya mwalimu kupata mafunzo ya ziada (capacity building) awapo kazini imekuwa na tatizo la muda mrefu ambalo kwa miongo kadhaa ngazi nyingine za watendaji wamekuwa wakipata lakini walimu.


>>>>>>>>>> 




Post a Comment

 
Top