0

PHOTO: Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.

Katika hali ambayo baadhi ya watanzania wanaofuatilia hali ya kisiasa na utendaji wa baadhi ya viongozi na watendaji wa sekta mbalimbali ndani ya serikali ya awamu ya tano,  wanafuatilia kwa karibu na kuangalia nini kinafuatia na kujua kwa undani zaidi kujiuzuru kwa aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini pichani juu.

Habari kutoka katika mkutano wa Waziri huyo na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam muda mfupi uliopita zinasema kiongozi huyo ameamua kubwaga manyanga kwa ambazo yeye mwenyewe amesema  ni kuipa nafasi serikali kufanya nchi iende mbele na si malumbano.

"sasa ni lazima kika kitu kiwe na tamati,  ninadhani mimi naweza kuwa sehemu ya suluhisho la malumbano yasiyokuwa na mwisho" alisema Prof. Muhongo.

Hata hivyo ameamua kujiuzulu kwake na kile alichotaja kuiachia serikali na Bunge kusitisha malumbano ya sakata la uchotwaji wa fedha katika account ya Escrow  akidai inaonekana yeye ni tatizo na kizingiti kupata muafaka. 

Post a Comment

 
Top