0
PROFILE PHOTO: Hali inaweza kuwa kama hivi kwa mabasi mengi kubaki katika ofisi zao hama kupaki katika stendi za mikoa pasipo kufanya safari.


DAR ES SALAAM.
Chama cha wamiliki wa Mabasi nchini (TABOA) kwa kushirikiana na Wamiliki wa Malori, Chama cha vyama vingine vya wasafirishaji mikoani kikiwepo cha mkoa wa Dar es Salaam kimewaomba wadau wao nchi nzima kuwaunga mkono baada ya kutangaza kufanya mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo nchi nzima kuanzia tarehe 03.05.2017 siku ya jumatatu ili kushinikiza serikali kutopitisha sheria ya usafirishaji inayotarajiwa kusomwa mara ya tatu na kupitia wabunge wa bunge linalotarajia kukaa hivi karibuni.

PROFILE PHOTO: Hii ni hatua ambayo inaweza kutazamiwa kujitokeza siku ya jumatatu endapo ufumbuvi hautafanyika mapema, hivyo kupelekea abilia wenye umuhimu wa kuelekea walipopanga kwenda kutumia miguu.


Akitoa maazimio hayo yaliyofikiwa katika mkutao mkuu maalumu wa chama cha wamiliki wa Mabasi, Malori, Daladala na Baji, katibu mkuu wa TABOA Eneo Mrutu amesema kuwa sheria hiyo inayotarajiwa kupitishwa haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki wa chombo cha usarishaji, hivyo hali inayosababisha kosa lililofanywa na dereva linapeleke mmiliki kuchukuliwa hatua za kufungwa jela pamoja kulipa faini.

Aidha amewaomba wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao kutopisha
sheria hiyo pindi itakapoletwa bungeni mpaka pale itakapofanyiwa marekebisho vinginevyo sheria hiyo inalenga kuvuruga sekta ya usafirishaji hapa nchini.


03.04.2017
UPDATE: Nimefika kituo kikuu cha mabasi ubungo naona mabasi yanaondoka kama kawaiad na abilia huku njiani nikikutana na mabasi ya daladala yakiwa na abilia wengi.


LAST UPDATE: KILICHOJILI HIKI HAPA CHINI: 





Post a Comment

 
Top