DAR ES SALAAM.
Abilia waliokuwa wakisafiri kutoka
mabibo kuelekea Makumbusho jijini Dar Es Salaam kwa kutumia usafiri wa daladala
walijikuta wakikataa kubebeana mabegi mara baada ya kusikia taarifa za kuwepo
kwa nyoka aliyeonekana ndani ya daladala katikati ya wiki hii jijini humo.![]() |
PHOTO: Haina uhusiano na
tukio katika habari hii.
|
Mwandishi wa habari hii ambaye alikuwemo
ndani ya gari hilo ambayo redio ya ndani ya gari hiyo ilikuwa ikitangaza (Clouds
fm) habari za nyoka huyo ambaye alioneka kwenye gari lenye namba za usajili
T184 DDJ lililokuwa likifanya safari zake kutoka Kibamba na Makumbusho jijiji
Dar, hivyo kupelekea abilia waliokuwa wamekaa kugoma kuwabebea mikoba abilia
waliokuwa wamesimama.
Msomaji wa taarifa hiyo alipomaliza kusoma
baadhi ya abilia walianza kukaguana kuona iwapo ndani ya daladala hilo kuna
aliyebeba begi kubwa linaloweza kuhifadhi mdudu huyo, ambapo watu wengi
waliokuwemo kwenye daladala hilo walionyesha kushtushwa na taarifa hiyo.
Wakati watu kadhaa walihusisha tukio
hilo na Imani za kishirikina wengine walisema huenda mmiliki wa joka hilo
alikuwa akilifuga. Katika tukio la daladala la Kibamba abiria waliokuwa ndani
ya gari hilo walisema tukio hilo la kutisha lilisababisha abilia kutaka kuruka
wakati likiwa kwenye mwendo wa kasi.
Source: Tanzania Daima.
Post a Comment