Tukio la kutekwa nyara kwa msanii wa
nyimbo za bongo freva Ibrahim Musa maarufu kama Roma Mkatoliki na wenzake wanne
waliokuwa Studio za Tongwe Records iliyopo masaki Dar Es Salaam wakifanya kazi
ya kurekodi nyimbo umefanyika ndani ya muda mfupi wa dakika 15 ambao watekaji aliutumia
kuingia na kuwachukua wasanii hao.
 |
PROFILE PHOTO: Ibrahim
Musa aka Roma Mkatoliki.
|
Watu hao ambao walikuwa na siraha
waliondoka na mateka huku wakitumia gari aina ya Toyota Noah ambayo shuhuda wa
tukio hilo aliyejulikana kwa jina maarufu Ze City alisema jinsi utekaji huo
ulivyofanyika.
Haika Shabani au ‘Ze City’ alisema
watekaji hao walifika katika studio hizo majira ya saa 12:30 jioni na kuongea
na Roma kwa takribani robo saa na waliondoka saa 12:45 baada ya kumuingiza Roma
na wenzake kwenye gari iliyokuwa na rangi nyeupe.
“Nilipokuwa
nashuka kwenye bajaji, ikaja gari nyuma yangu, ikashusha watu watano,
wakatuamuru tuliokuwa nje nikiwamo mimi, producer na watu wengine wawili
tuingie ndani, baadaye walituambia bila kujitambulisha kuwa wamekuja kumtafuta
J Murder ambaye ni mmiliki wa studio hiyo na Roma, wakaambiwa wamemkosa mmiliki
ila Roma yupo”
alisema Ze City.
Aliongeza kuwa “baada ya kuitiwa Roma na kutoka naye nje
na kuingia naye kwenye gari, wachache waliingia studio na walipotoka walibeba
TV na CD zilizokuwepo pale ambapo baadaye walirudi naye ndani na kuchukua
baadhi ya vitu kama camera na kuondoka na watu wawili akiwamo mlinzi na msanii aliyefahamika
kwa jina la Moni.”
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar Es
Salaam Simon siro tayari aliunda kamati maalum kufuatilia na kucunguza tukio
hilo, huku zikiwa tayari zimetimia siku mbili tangu msanii huyo kutekwa. Wakati
huohuo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa taarifa kwa vyombo
vya habari kuwa inafuatilia kwa karibu suala hilo na imebaini ni la kijinai.
Vilevile hapo jana wasanii wapatao 30
waliungana kupaza sauti zao kutaka mamlaka husika zichukue hatua stahiki ikiwa
ni zaidi ya saa 40 kupita tangu alipotekwa muimbaji huyo wa nyimbo za kufoka.
Source:
Mwananchi
 |
PROFILE PHOTO: Kamanda
wa Polisi kanda
maalum ya Dar Es
Samaa Simon Siro.
|
Mara baada ya tukio hilo kugusa hisia za
watu mbalimbali Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam Simon Siro
ametoa taarifa na kuwa leo asubuhi
katika kituo cha polisi Oystebay jijini
Dar Es Salaam mwanamuziki huyo Roma Mkatoliki alifika katika kituo hicho mara
baada ya kuachiwa na watekaji hao.
“Baada
ya yale mahojiano wengine wakawa wanawahoji kwa kutumia nguvu, wana majeraha
kidogo ambayo yameonekana hivyo baada ya kuwahoji wameonekana kupaniki wamechukuliwa
maelezo yao na nimeelekeza wapilekwe hospitali na askali wetu wa upelelezi.” Amesema Kamanda
Siro.
Aliongeza kuwa “kimsingi niseme kuwa wote wanne
wamepatikana wakiwa salama na upelelezi wa kina unaendelea kwa wote waliohusika
na hilo tukio ingawa wanasema hawakuwatambua lakini zile zilikuwa taarifa za
awali baada ya kuwa watakuwa wametulia watatupeleka katika eneo la tukio
tuendelee na upelelezi na baadaye tutajua kwa undani kuhusu tukio hili.”
LATEST: Muda mfupi baada ya kutoka hospitali, mwanamuziki huyo alisema "Mimi ni mzima kabisa kiafya" ikiwa ni baada ya kufanyiwa vipimo katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar Es Salaam ambapo amesema atazungumza mengi siku ya Jumatatu.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.