0
DUBAI. 
Moto mkubwa umetokea mapema leo Jumapili katika jengo refu lilokuwa bado linajengwa karibu na eneo kubwa la biashara (Dubai shopping mall), na kueneza moshi mzito angani uliolifunika eneo kubwa katikati ya jiji.


Eneo hilo la ujenzi lilioko jirani kabisa na Dubai Mall na karibu na Jengo lefu lenye ghorofa 63 linalojulikana kama The Address Downtown Dubai Tower, ambalo liliharibiwa vibaya sana na moto wakati wa kilele cha mwaka mpya 2015.

Jengo hilo refu lijulikanalo kama Fountain Views Complex linajengwa na mwekezaji mkubwa wa Dubai, Emaar Properties ambae alijenga Mall na hoteli ambayo ilishika moto mwaka 2015. Mwekezaji huyo alikataa kutoa kauli yoyote kuhusu ajali iliyotokea leo.

Miale ya moto ilikuwa ikilindima katika jengo hilo wakati wazima moto wakirusha maji ndani ya kusaidia kuzima moto. Kila dakika chache, kulikuwa na milipuko inasikika ndani ya jengo.

Vyanzo vya habari vinasema inafikiriwa kuwa miripuko hiyo inatokana na mitungi ya gesi iliyokuwa inatumiwa na wafanyakazi.

Magari ya kubeba wagonjwa yalikuwa yamesimama karibu na jengo ili kutoa huduma ya kwanza lakini hakukuwa na dalili kama kuna mfanyakazi yoyote aliyehitaji matibabu au huduma ya kwanza. 
Moto ulionekana kuwa umedhibitiwa katika ghorofa za chini katika jengo hilo.

“Huduma za kupooza joto katika jengo hilo zinaendelea na magari ya kubeba wagonjwa yako tayari katika eneo hilo,” ofisi ya habari ilituma ujumbe huu katika akaunti yao ya Twitter ambapo imesema hakuna majeruhi walioripotiwa.


Source: voa

Post a Comment

 
Top