Baadhi ya matukio katika picha wakati wa kuhitimisha mafunzo ya walimu wanaojiandaa kufanikisha mafunzo ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa mtaala ulioboreshwa kwa nchi nzima kwa wanafunzi wa darasa la tatu na nne.
 |
PHOTO: Naibu waziri wa Elimu na Ufundi
Injinia Stella Manyanya akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili katika chuo cha Ualimu Bustani Kondoa.
|
 |
PHOTO: Naibu waziri Injinia Stella Manyanya (katikati)
akiwa na viongozi wa mkoa wa Dodoma, mkuu wa wilaya ya Kondoa Kijazi (wa pili
kushoto), viongozi wa mafunzo, Mkuu wa chuo cha Bustani wakielekea Ukumbuni
kuhitimisha mafunzo ya Awali kwa walimu.
|
 |
PHOTO: Wahitimu wapatao 444 ambao walihitimu
mafunzo ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu pamoja na Kuchopeka wakiwa makini
kufuatilia kile kinachoendelea wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
|
 |
PHOTO: Dr. Siston Masanja, ambaye ni Mtendaji
mkuu wa ADEM akitoa taarifa fupi ya mafunzo tangu yalipoanza na kuhitimishwa
kwake ambapo jumla ya washiriki 444 walihitimu mafunzo, kulia kwake ni mkuu wa chuo wa Bustani.
|
 |
PHOTO: Sehemu ya sherehe yoyote ni nyimbo na
furaha, (Kwaya) Walimu wakiimba wimbo wa kushukuru kupata mafunzo na kuonyesha
hamasa kwenda kuyatumia kwa walengwa ambao ni wanafunzi wa darasa la 3 na 4.
|
 |
PHOTO: Baadhi
ya walimu wakipiga makofi mara kutokana na wimbo ulioimbwana kwaya ya walimu katika sherehe hiyo. |
 |
PHOTO: Kaimu Mkurugenzi mkuu, Taasisi ya
Elimu Tanzania Dr. Elia Kibga akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo
huku akigusia kuhusu ubora wa mafunzo hayo kwa mwanafunzi atakayemaliza awe
mwanafunzi bora na si bora mwanafunzi.
|
 |
PHOTO: Baadhi ya walimu wakifuatilia hotuba
kutoka kwa kaimu mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Elia Kibga (pichani juu)
|
 |
PHOTO: Mratibu wa Mafunzo kituo cha kutolea
Mafunzo cha Bustani Kondoa Luca Mzelela akiongea wakati wa kumkaribisha Naibu
waziri kufunga mafunzo hayo, kushoto kwake ni Naibu waziri Stella Manyanya na Mkuu wa wilaya ya Kondoa Kijazi.
|
 |
PHOTO:
Naibu Waziri wa Elimu Injinia Stella Manyanya akisisitiza kuhusu mafunzo
hayo ambayo ni nadra kutokea kwa walimu kutokana na ufinyu wa Bajeti, wakati wa
kuhitimisha mafunzo ya awali kwa walimu wa shule za msingi nchini katika kituo
cha Bustani Kondoa, kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kondoa -Kijazi.
|
 |
PHOTO: Wawezeshaji wanaotoa mafunzo ya KKK na
Uchopekaji wakimsikiliza Naibu waziri Injinia Manyanya wakati akihitimisha mafunzo hayo ya awamu
ya kwanza.
|
 |
PHOTO: Naibu waziri Stella Manyanya (kulia)
akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo Nurdin Ibrahim ikiwa ni kumbumbuku ya kuhitimu.
|
 |
PHOTO: Naibu waziri Stella Manyanya (kulia)
akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Zauda Hussein cheti cha kuhitimu mafunzo.
|
 |
PHOTO: Picha ya pamoja kwa mgeni rasmi akiwa
na viongozi wa ADEM na watoa mafunzo mara maada ya kuhitimishwa kwa mafunzo ya
awamu ya kwanza yaliyofsnyika mkoani Dodoma katika wilaya ya Kondoa kwenye chuo
cha Ualimu Bustani.
|
Picha: TODAYS PRODUCTION
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.