0
Chama cha wanasheria nchini (Tanganyika Laws Society) wanafanya mkutano wao kupitia ajenda muhimu za chama hicho jiji Arusha ikiwa ni pamoja na maandalizi ya mkutano mkuu  wa mwaka ukiwemo uchaguzi wa Rais wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa AICC jini hapa.

Chama hichi kina wanachama walioandikishwa katika daftari wapatao 6000 huku jumla ya wanachama wanaokadilia kufika 3000 wameudhulia mkuano na ambao wanategemea kuchagua viongozi huo na kwa mujibu wa kanuni za chama hicho uongozi hudumu kwa mwaka mmoja ambao wanategemea kuongoza chama hicho kwa mwaka mmoja ujao wa chama hicho cha (TLS).

Wakati mmoja wa wagombea ambaye kwa wiki nzima amekuwa akitajwa sana kutokana na kampeni zilizoanza, kwenye uchaguzi unaofanyika kesho wagombea wapato sita Voctoria Mandare, Francis Stora, Tundu Lissu, Godwin Mwapongo na Laurence Masha wanatarajia kuchuana katika nafasi ya urais wa Chama cha wanasheria nchini TLS.

Hata hivyo Rais anayemaliza muda wake John Sekka ameshukuru wananchama wa chama hico huku akisifu maendeleo aliyofanya ya ukusanyaji wa fedha ili kuwekeza katika jengo la chama hicho, huku uboreshaji wa huduma kwa wanachama pamoja na mahusiano mazuri na serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais John Pombe Magufuri ikiwemo idara iliyo upande wao idara ya mahakama.

Hapa chini nakuwekea picha kadhaa za wanasheria waliofika katika mkutano huu ambao kwa haki halisi mpaka sasa ukumbi wa mkutano umejaa na bado kuna wanasheria nje ya ukumbi.











Post a Comment

 
Top