0
PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akiongea
wakati wa uzindizu wa kampeni ya wananchi kutoa maoni.
Na. Mary Mwakibete MBEYA.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amezindua zoezi la wananchi kutoa maoni juu ya migogoro ya Aridhi na mipaka ya vijiji 34 pamoja na hifadhi ya Ruaha ambapo katika uzinduzi huo alifanya mikutano kadhaa katika vijiji kadhaa kikiwepo kijiji cha Igava  kata ya Igava wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya.

Katika uzinduzi huo ametambulisha timu mbili za wataalam watakaopita katika vijiji hivyo 34 kupokea maoni ya wananchi  ikiwa ni baada ya wananchi kulalamika kuwa mwaka 2008 wakati serikali inatangaza mipaka wananchi hao hawakushirikishwa, ambapo kupitia mkutano huo mkuu huyo wa mkoa amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi pale ambapo kamati hiyo itakuwa inapita katika vijiji vyao.

Baada ya wananchi kutoa maoni baraza la madiwani, kamati ya ushauri ya wilaya watatoa maoni na baadaye kamati ya ushauri mkoa na hatimaye kuwasilishwa kwa muheshimiwa Rais kwa ajili ya maamuzi.

RC Makala amewaonya wale watakaohujumu zoezi hilo muhimu kwani lengo la zoezi hilo ni kuondoa mgogoro na hifadhi lakini utasaidia kuboresha ekolojia ya hifadhi ya Ruaha.


Wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amewaomba waviongozi wa dini na Kimila kusaidia kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa ajili vya uraia pia kuwaepusha na Imani potofu, ambapo amewaomba viongozi hao kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya Uraia huku akiwataka viongozi kuwa macho na watu wasiokuwa Raia kuweza kuandikishwa kutokana na Mkoa huo kuwa mpakani hali inayoweza kutoa fulsa wasio raia kujiandikisha.


PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mwenye suti na tai nyekundu akiwa na baadhi ya viongozi mbalimbali mkoani Mbeya.

Post a Comment

 
Top