MUSOMA.
Ushuri huo umetolewa na
Graca Machel aliyewahi kuwa mke wa Rais wa msumbiji hayati Samora Machel pia
baadaye alikuwa mke wa aliyepata kuwa Rais wa Afrika kusini Nelson Mandera,
ambapo aliwasili mkoani humo machi 13 kwa ziara ya siku tatu mkoani Mara
kuangalia maendeleo ya mradi wa kusaidia watoto walio nje ya mfumo wa Elimu,
unaotekelezwa na taasisi yake.
Mama Machel alitoa
ushauli huo wakati wa mkutani maalum na wadau ambapo katika mkutano uliotumika
kutoa matokeo ya utafiti wa watoto ambao wapo nje ya mfumo wa shule. Pia
utafiti huo umebaini watoto wapatao 11,666 wenye umri kati ya miaka 7 hadi 17
wapo nje ya mfumo wa shule chini ya mradi wa miaka miwili ambao unatekelezwa na
taasisi ya Graca Machel Trust kwa ushirikiano na Mara Alliance na Serikali ya
mkoa kwa Mara.
![]() |
PHOTO: Mama Graca Machel (wa pili kushoto) akiongoza na Askofu Michael Msongazila wa jimbo la musoma na Mwenyekiti wa Alliance.
|
“Tunahitaji mpango wa miaka mitano au kumi na tano ili kuondoa
ili tatizo na huu ni mwanzo wa safari kuondoa tatizo la watoto ambao wako nje
ya mfumo wa shule” alisema Mama Graca Machel.
Pia utafiti huo
umeonyeshwa katika halmashauli tano za wilaya za Tarime, Bunda Musoma na
Butiama, kupitia wilaya Bunda umeonyesha inaongoza kuwa na watoto wengi walio
nje ya shule kwa asilimia 33, Tarime (31), Butiama (26) na M usoma (10). Mkuu
wa kitengo cha utafiti na machapisho ya utafiti wa masuala ya uchumi na Jamii
(ESRF) ambao wamefanya utafiti huo Dkt Fortunata Makene alisema, utafiti huo
umefanyika nyumba kwa nyumba.
Dr. Makene alisema ni
muhimu kuwepo na mpango wa kukabiliana na tatizo la ndoa za utotoni katika mkoa
wa Mara.
Kwa upande wake mdau wa
elimu mkoani Mara, Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Musoma Michael
Msonganzila alisema kuwa , ni habari njema kuona GMT , Mara Alliance na
Serikali wameungana kusaidia watoto ambao wako nje ya mfumo wa elimu ya shule
chini ya mpango wa Memkwa.
Akizungumza katika
hafla hiyo kaimu mkuu wa mkoa wa Mara , Dr Vicent Naano alimhakikishia mama
Graca kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kuwa
tatizo la watoto walio nje ya mfumo wa shule linabaki kuwa historia na kufanya
mradi huo kuwa wa mafanikio makubwa.
Chanzo: Habari Leo.


Post a Comment