| PROFILE PHOTO: Rais John Pombe Magufuri. |
Mmoja wa wahasisi wa Uhuru
na aliyewahi kuwa mmoja wa watendaji wakuu katika serikali ya Tanganyika Sir
George Kahama amefariki dunia Jumapili iliyopita akiwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili alipokuwa akitibiwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na ofisa uhusiano
wa hosptali hiyo.
Rais John Magufuli alituma salamu kwa wafiwa pamoja na
rambirambi zake kwa familia akisema taifa limempoteza mmoja wa watu muhimu na
aliyetoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru, maendeleo na ustawi wa jamii ya
watanzania. Pia Dkt Magufuli amewapa pole wanachama wote wa CCM, wabunge,
ndugu, na marafiki pamoja na wote walioguswa na msiba huo.
Dkt Magufuli amesema, "Sir George
alikuwa kiongozi mzalendo,shupavu na mwanasiasa mahiri, aliyewapenda watanzania
lakini pia alijitoa kushirikiana na viongozi wenzake akiwemo Baba wa Taifa
hayati Mwalimu Julius Nyerere pia alipigania uhuru, kujenga misingi ya taifa
likiwemo Azimio la Arusha ikiwemo kujenga misingi ya uchumi wa ujamaa na
kujetegemea, kwa hakika hatutamsahau"
Post a Comment