DAR ES SALAAM.
Kabla ya uzinduzi na kuweka jiwe la msingi
la ujenzi wa barabara za mwingiliano na kupishana (frying over/Interchange)
kwenye eneo la Ubungo muda mfupi uliopita Rais Magufuri aliwaelezea watanzania
yaliyofikiwa ndani ya kipindi chake cha uongozi aliopo ikiwa ni pamoja na
baadhi ya watu waliokuwa wanapiga kelele kuhusu kusitisha sherehe za Uhuru na
fedha zake kuelekezwa kwenye ujenzi wa barabara ya Morocco -Mwenge.
Kutokana na hilo
amesema wote waliokuwa wanapiga kelele kuhusu fedha za sherehe hizo sasa
wanawahi kufika ofisini kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Aitha ameelezea
masikitiko yake kwa watu kujielekeza mno katika masuala ya udaku ambayo hayana
tija kwa taifa na hayaongeze chochote, hayatusaidii chochote na ndio
yanayochukua muda mwingi, kufuatia hilo amesema "tuzungumze uchumi,
tujielekeze katika mambo ya maendeleo ambayo hayana chama na nimefurahi kumuona
mstahiki meya ambaye ni wa CHADEMA"
Pia aliongeza kwa
kusema "Kampeni zilishakwisha, ulie ugalegale Rais ni
Magufuli. Ndio maana hii interchange inajengwa kwenye jimbo la Chadema na
nawaomba watanzania wa vyama vyote tujielekeze kwenye suala la maendeleo, aliongeza kwa kusema “mnaangaika
kwa kuposti kwenye vipost vyenu, mpaka watu wengine wanaingilia uhuru wangu,
mimi huwa sipangiwi mambo”.
Alisisitiza kuwa
yeye ni Rais anayejiamini na huwa awezi kupangiwa maana hata siku ya kuchukua
fomu alienda mwenyewe, hivyo ataamua mwenyewe nani akae wapi, kwa hivyo alisema
“Makonda wewe chapa kazi, nasema chapa kazi, nafahamu
wamenielewa kama ni kuandikwa kwenye mitandao haina tija, hata mimi naandikwa sana
kwenye mitandao kwahiyo nijiuzulu Uraisi?
Hata hivyo Rais
aliongeza kuwa angefurahi endapo kwenye mitandao watu wangekuwa wanatoa ushauri
kuwa nini kifanyike na siyo kujadili personality badala ya ideas na alisem
tuchape kazi kwa manufaa ya watanzania wote.


Post a Comment