Mkurugenzi wa Clouds
Media Ruge Mutahaba ambaye ka nafasi yake anasimamia vipindi, mapema leo
asubuhi amezungumza sakata la Kituo hicho kuvamiwa na askali polisi wakiwemo
wengine waliovalia magwanda ya jeshi la wananchi nchini uvamizi uliofanyika
usiku majira ya saa 5 kasoro ijumaa iliyopita.
DAR ES SALAAM.
Akizungumza
kupitia kipindi cha 360 amesema kitendo hicho alichofanya mkuu wa mkoa wa Dar
Es Salaam Paul Makonda si cha kiungwana ikizingatiwa kuwa kiongozi huyo mkuu wa
nchi ni rafiki yao wa karibu, hivyo kwenda katika studio hizo na askali wakiwa
na siraha kuliwatia hofu wafanyakazi wa chombo hicho.
“Nilimpigia simu Makonda kumhoji kwa nini aje ofisini na
maaskari wenye siraha? Yeye akauliza kwa nini nimezuia kipindi kuruka?, kisha
Makonda alikata simu, lakini nilipaniki nikiwaza kuhusu hizo siraha walizokuja
nazo ofisini, makonda alisema ‘Bahati yenu’ baad ya kujua kuwa vijana wa
SHILAWADU waliokataa kurusha kipindi siyo wao isipokuwa ni mimi” alisema Ruge.
Sakata hilo la mkuu wa
mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kwenda katika kituo hicho kwa kuvamia na
askari kimetokana na moja skendo ya kutengeneza ambayo imetokana na mama mmoja
ambaye alipiga simu katika kituo hicho na kudai kuzaa ma Bishop Gwajima ambapo
baada ya kufuatilia (balance story) inasemekana haikuwa kweli, hivyo kutokana
na kitendo cha Bishop Gwajima kumuweka wazi mkuu wa mkoa kuwa hatumii jina lake
halisi ahli hiyo imepelekea mkuu huyo wa mkoa kutaka clip hiyo iliyorekodiwa
kurushwa ili watu wajue kitendo anachofanya mchungaji huyo wa kondoo.
Aitha Ruge aliendelea
kusema kuwa alimpigia simu Kusaga ambaye ni Mkurugenzi wa Clouds Media na
kumwambia mkuu wa mkoa ametukosea heshima kwani kulikuwa na aja ganiaje na
silaha na ni rafiki yetu?, pamoja na kwamba hakuna aliyepigwa lakini kulijengwa
hofu kubwakwa wafanyakazi wa Clouds Media si Jambo dogo.
Ruge alisema “kama watanzania
hatutaki kuona kuiona bunduki mitaani, hili limetokea kutufungua macho kujua
ma-RC na ma-DC wanavyofanya kazi yao, sisi tuhukumiwe kama taasisi, wafanyakazi
wetu wasitiwe hofu, mimi sikuwekwa ndani, nilienda polisi kuripoti suala hili,
mtu kuwa na nafasi ya uongozi flani si sababu ya kuwapanda watu, All we want is
Respect!”
Kituo hicho cha habari
CloudsMedia kinalaani kilichotokea na inaomba vyombo vya Habari vitoe
ushirikiano katika kukemea jambo hili.

Post a Comment