0
Mambo mengi yamejitokeza hivi sasa kuhusu mtu mwenye umri wa miaka 52 ambae aliwaua watu wanne Jumatano na kuwajeruhi watu zaidi ya 12 wengine katika Daraja la Westminster na ndani ya Jengo la Bunge la Uingereza.

PROFILE PHOTO: Khalid Masood akiwa anapewa huduma ya
kwanza marabaada ya tukio la mashambulizi.

ILIPOISHIA:....
Muuaji huyu alilaumu ubaguzi kwa kupigana kwake, akiiambia mahakama alimkata mmiliki wa mgahawa huo usoni kwa sababu watu wa eneo alilokuwa anaishi katika kijiji cha East Sussex 
“walimuonyesha chuki” wakati huo alipokuwa anaishi huko.

UPDATE: Endelea hapa,
Jaji aliyemhukumu alitoa angalizo: “Wakati huna fursa ya kutoa kisingizio chochote kwa tabia yako, inaweza kutoa maelezo kwa kiwango fulani .”
Lakini tabia yake ya uvunjifu wa amani katika takriban kesi zote zinazohusu maeneo yote ya umma dhidi yake kwa miaka mingi ziliendana na tabia yake ya ulevi kabla ya tukio la mwaka 2000 katika ugomvi wa kwenye baa ambapo alikuwa amekunywa pint nne za bia.

Wakati historia ya utotoni na saikolojia ya Khalid Masood ina umuhimu kwa wataalamu wa misimamo mikali (na vyombo vya habari vya Uingereza), ambao wanataka kujua nini kilimpelekea kuuwa, hilo ni jambo dogo kwa wachunguzi wa polisi ambao wana maswali yanayo husu matukio ya sasa na maswali muhimu ambayo yanahitaji majibu kati ya hayo, ni lini, kwa nini, na vipi alikuwa ameingizwa katika misimamo mikali.

Wakati polisi wakipekuwa historia ya Maisha yake ya siku za nyuma, wanataka kugundua mara moja kama alifanya hilo shambulio kwa uamuzi binafsi au alikuwa ameelekezwa kulenga Bunge la Uingereza na Je alikuwa ni sehemu ya mtandao wa watu wenye misimamo mikali ambao wanaendelea na mipango ya mauaji?

Miaka miwili akiwa Gerezani.
Tarehe za kubadilisha kwake dini kuingia Uislamu hazijulikani, lakini inadhaniwa kuwa aliingia katika siasa kali wakati akitumikia kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kumkata mtu na panga mwaka 2000 alipokuwa  baa,katika nchi kadhaa za Ulaya, wengi ambao wanaingizwa katika siasa hizo kali ni wale ambao waliwahi kutenda vitendo vya jinai.

Hakuna mafungamano ya makundi ya wahalifu na kikundi cha Islamic State au makundi mengine ya wapiganaji lakini yako mafungamano fulani ya makundi ya kijamii, mazingira na vijana kwa makundi ya wahalifu na magaidi huwapata wafuasi wao katika makundi hayo, wakitengeneza mahusiano, wanasema wachambuzi.
Watu ambao walifanya mashambulizi kwenye jiji la Paris mwaka 2015 na kwenyue jiji la Brussels walikuwa na historia ndefu ya utukutu utotoni mwao na baadhi yao wanajulikana kuwa waliingizwa katika makundi hayo wakati wakitumikia kifungo jela, au waliingizwa na watu ambao walikuwa wameambukizwa siasa kali wakati wakiwa jela.

Tangu siku ya Jumatano polisi wamekuwa wakipekua nyumba kadhaa ndani ya Uingereza na wamewakamata watu 11 mpaka sasa, wengine kama ni washukiwa wanaojihusisha na kuandaa vitendo vya ugaidi. Kati ya hao ni mtu mwenye umri wa miaka 27 kutoka Birmingham na mwanamke, miaka 32, kutoka Manchester.

“Wote hawa wanahojiwa wakati tukijaribu kuunga vipande vya taarifa tulizokusanywa katika kile kilichotokea katika shambulio hilo,” afisa wa ngazi ya juu wa polisi ameiambia VOA. Uchunguzi huo wa polisi, unaoitwa “Operation Classific” unaongozwa na maafisa kutoka SO15, Kikundi cha kupambana na ugaidi cha Polisi, Jijini London.

Kaimu Kamshina Msaidizi Mark Rowley Ijumaa amesema: “Hivi sasa hakuna ushahidi wa tishio lolote zaidi lakini utaelewa kuwa nia yetu ni kujua iwapo alitenda haya peke yake na kushawishiwa na propaganda za magaidi; au, watu wengine wamemsaidia, wamempa moyo na kumuelekeza afanye hivyo.”

Dakika tatu kabla ya kuendesha gari aina ya Hyundai SUV alioikodi na kuwagonga watembea kwa miguu, alioipeleka upande wao wakati wanatembea kuvuka daraja la Westminster Bridge, Khalid Masood alikuwa amefanya mawasiliano na mtu kupitia WhatsApp.

Polisi wanajaribu kumtambu mtu huyo alikuwa ni nani na walikuwa na mazungumzo ya aina gani.

PROFILE PHOTO: Polisi wa jiji la London wakifanya uchunguzi kutokana
na tukio la ugaidi la shambulizi lililofanywa na khalid-Masood.
Miaka aliyokuwa Saudi Arabia
Alikokuwa anaishi katika siku za nyuma kumewafanya wachunguzi kutaka kujua zaidi. Kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa London walio ongea na VOA, Khalid Masood inasadikiwa aliwahi kuishi kwa miaka kadhaa Saudi Arabia.
Gazeti la The Sun limeripoti kuwa alihamia nchi hiyo mwaka 2005 na kwa miaka minne aliwafundisha kiingereza wafanyakazi wa taasisi ya usafiri wa angani huko Yanbu.

Je, Saudi Arabia ndiko alikobobea katika msimamo mkali?
Mwaka 2009 alihamia Luton, kaskazini mwa London ambako tena alikuwa anafundisha Kiingereza, part-time. Kuchagua kwake kwenda Luton kunaweza kuwa na umuhimu fulani kama ilivyokuwa uamuzi wake wa kuhamia Birmingham. Miji hiyo miwili imeonyesha wazi kuweko kwa kikundi cha kigaidi cha Islamic State chenye kuwaingiza raia wa Uingereza kwenye ugaidi.

Washambuliaji waliotumia mabomu July7, 2005 jijini London walikuwa na mafungamano na mji huo na miji yote hiyo imekuwa ikitembelewa na wahubiri wenye siasa kali, kwa siku za nyuma akiwemo Abu Hamza, Omar Bakri Mohammed na Anjem Choudary ambae ni muhubiri maarufu mwenye siasa kali aliyefungwa mwaka jana kwa makosa ya ugaidi na amehusishwa na njama za kupanga vitendo vya ugaidi mara 15 tangu mwaka 2000.

Ilikuwa wakati yuko Luton na Birmingham, ndipo vyombo vya upelelezi vya Uingereza vilipoanza kumfuatilia Khalid Masood, alionekana pia na majirani zake huko Luton kama “mkazi,” lakini mmoja wa majirani zake alimuelezea kwa waandishi wa Uingereza alikuwa anaishi kama “kivuli.”

“Sikuwa namuona mara kwa mara, mara nyingine namuona akitembea usiku, sikuwahi kumuona mchana kwani ilikuwa tabu kujua anaishi eneo hilo.” Kwa polisi wa Uingereza wasiwasi wao ni kuwa inawezekana walipitwa na umuhimu wa kuwatambua “majirani hatari” wengine.


TUISHIE HAPA KWA LEO.
Kwa maoni tuandikie hapo chini kwenye comment au WhatsApp +255773036064





Source BBC.

Post a Comment

 
Top