0
Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA inaendesha mafunzo ya utoaji wa taarifa za dawa bandia mkoani Arusha kwa wataalam wa afya nchini ikiwa ni sehemu ya mafunzo yanayofanywa nchi nzima ikiwa ni sehemu ya kupunguza na kuondoa dawa zisizo halisi katika matumizi ya dawa zinazotakiwa kutumika kwa binadamu.


Kaimu meneja wa Chakula na dawa kanda ya kaskazini Abdallah Mkanza akiongea na TODAYS NEWS juu ya mafunzo ha utumiaji wa simu katika kupeleka taarifa za madhara na kuwepo kwa dawa duni bandia.

Mkufunzi wa mafunzo ya matumizi ya program tumishi ya MPRO5 Elia Nyeula akieleza kwa undani juu ya mfumo huo mpya.

Wauguzi na watoa tiba kutoka mkoa wa Arusha wakifuatilia mafunzo
hayo mapema jana katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Arusha.
Madaktari wa wataalam wa Afya kutoka vituo vya Afya na Hospitali
kadhaa za mkoa wa Arusha wakiwa makini kufuatilia mafunzo.

Picha ya pamoja kwa wauguzi, madaktari, mkufunzi na mgeni rasmi katikati kabla ya kuanza mafunzo hayo jijini Arusha mwishoni mwa wiki hii.




HABARI KWA UNDANI:


ARUSHA.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyowashirikisha wataalam wa Afya wakiwemo madaktari na wauguzi kutoka wilaya za mkoa wa Arusha wamepewa ujuzi wa kutambua dawa duni na bandia huko ziliko pamoja na kuweza kuzipiga picha na kuweza kutuma taarifa kwa wakati kwenda kwaa mamlaka husika kupitia program tumishi  ambayo inapatikana kupitia mfumo wa simu za kiganjani (smartphone).

“TFDA ikishirikiana na shirika la Afya duniani (WHO) inaendesha  mafunzo  baada ya kuona kuna umuhimu kutokana na kukua kwa teknolojia, hivyo matumizi ya kutumia simu za kisasa (smartphone) yatarahisha mtu kuweza kupiga picha na kuituma kwetu nasi kwa muda na wakati tutakuwa tumeokoa watanzania wengi ambao wangeweza kutumia dawa hizo duni na bandia” amesema Abdallah Mkanza kaimu meneja wa mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kaskazini.

Wakati mafunzo hayo yakiwa ni ya mwisho yakihitimishwa kwa nyanda ya kaskazini baada ya kufanyika nchini kote, hata hivyo kumekuwepo na malalamiko kutokana na matumizi ya dawa za ARV–TLE ambazo baadhi ya watumiaji wamekuwa wakiwashwa  na kubabuka baada ya kutumia dawa hizo, tatizo hilo linaonekana ni kubwa lakini tfda tunaendelea kufanyia kazi, aliongeza Mkanza.

Mkaguzi wa dawa kiongozi nyanda ya kaskazini Elia Nyeula anayeendesha mafunzo hayo anasema, mafunzo hayo yanayowajumuisha wataalam kutoka katika hospitali hapa nchini ni nzuri na ya haraka katika utoaji wa taarifa hizo muhimu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa dawa duni na bandia zinaondoka.

“kwa nchi za Afrika na dunia kwa ujumla program hii ndiyo inaanza na itztusaidia sana Tanzania nasi tumechukuliwa kama pirot (viongozi) ili wengine wajifunze kutoka kwetu. Swala la madawa bandia na yaliyo chini ya kiwango ni tatizo la kidunia, siyo Tanzania tu lakini kutokana na teknolojia kuongezeka lakini pia watu kutaka kujiongezea uchumi wao binafsi” anasema Elia Nyeula.

Aliongeza kuwa kunapokuwepo kwa dawa bandia kunahafifisha nguvu kazi lakini pia uchumi wa nchi, ambapo tunapotoa mafunzo haya kwa wataalamu hawa watakuwa ni chachu kwenye sehemu zao za kazi na kwa taifa kwa ujumla.

Program hiyo tumishi inapatikana kwa kupakuliwa kupitia simu za kijangani (smartphone) inajulikana kwa jina mpro5 itaaanza kutumika kwa wataalamu wa Afya ambao watakuwa na namba maalum ambazo zitawasaidia kuingia na kutoa taarifa.


“Nina imani haya mafunzo yatatusaidia kwani wateja wetu ambao ni wagonjwa wamekuwa wakilalamika kutokana na kuwepo kwa dawa bandia, hivyo mafunzo haya yatatusaidia kuweza kutoa elimu vituoni, kutoa taarifa baada ya kuona madhara ya dawa bandia maana huwezi kutoa taarifa wakati hujaona madhara yaliyotokana na matumizi ya dawa hizo pia kuweza kuepukana na hili janga” amasema afisa muuguzi msaidi Josebetina Kamugisha kutoka kituo cha Afya Levolosi Arusha.

Post a Comment

 
Top