![]() |
PHOTO:
Mimbari ya msikiti ikionekana kwa nje.
|
Kulikuwa na hisia kali katika bunge la Israel siku ya Jumatano wakati lilipopitisha sheria kuzuia vipaza sauti miongoni mwa taasisi za kidini, matoleo mawili ya muswada huo uliojulikana kama ''muswada wa Muezzin'' ambao ungeathiri wito wa ibada miongoni mwa Waislamu 'Adhan' ulisomwa kwa mara ya kwanza na kupitishwa na wachache.
Baadhi ya wabunge wenye asili ya uarabuni
walizichana chana baadhi ya nakala za muswada huo wakati wa mjadala uliokuwa na
changamoto, hivyo kupelekea muswada huo ambao utalazimika kusomwa kwa mara nyingine
na kupitishwa kabla ya kufanywa sheria.
![]() |
PHOTO: Taswira
ya anaye *Adhin kuwakumbusha waumini kwenda kwenda ibada.
|
Ni marekebisho ya muswada
ulioidhinishwa na baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu mnamo mwezi Novemba
mwaka uliopita, ambapo Netanyahu alisema kuwa amepokea malalamishi kadhaa kutoka
katika jamii zote za Israel kuhusu kelele na matatizo wanayopata kutokana na
kelele hizo zinazotoka katika vipaza sauti.
Mmoja
ya watu wanaoupigia debe muswada huo Motti Yogev wa chama cha Jewish Home Party
alisema siku ya Jumatano kwamba ni muswada unaolenga kuwasaidia raia kupumzika ''Hatuna nia ya
kuwaumiza wafuasi wa dini yoyote'', aliongezea.
Wakosoaji wa muswada huo wanasema
kuwa unakandamiza wa uhuru wa kuabudu, sauti ya ''Adhan'' haijawahi kusababisha
uchafuzi wowote wa mazingira, kwani mojawapo ya tamaduni za dini ya kiislamu na
hatujawahi kingilia sherehe yoyote ya kidini inayohusu Judaism.
“Vitendo vyenu ni vya kibaguzi'' ,alionya
Ahmed Tibi wa chama cha Joint List alliance chenye Waarabu wengi. ''hatua hii
inalenga Uislamu'', aliongezea.
Raia wa Kiarabu nchini Israel
wanaojulikana kama waarabu Waisraeli ni kizazi cha Wapalestina 160,000
waliosalia baada ya taifa la Israel kubuniwa 1984, wao ni asilimia 20 ya idadi
ya Waisraeli . Asilimia themanini ya Waisraeli Waarabu ni Waislamu na
waliosalia wamegawanyika sawa kati ya Wakristo na Druze.
Source bbc.


Post a Comment